SI KWELI Lamine Yamal mwenye miaka 17 ana mtoto wa miaka mitatu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Salaam Wakuu,

Nimekutana na taarifa inayodai kuwa Mchezaji Kinda wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Uhispania Lamine Yamal ana mtoto wa miaka mitatu.

Taarifa hii imenistua sababu Kinda huyu ametimiza miaka 17 siku mbili zilizopita (13/07/2024). Kuwa namtoto wa miaka mitatu inamaanisha alipata mtoto akiwa na miaka 13.

Upi ukweli hapa Wakuu?



 
Tunachokijua
Lamine Yamal ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Hispania mwenye asili ya Morocco na Guinea Equatorial. Alizaliwa tarehe 13 Julai 2007. Yeye ni kijana mdogo ambaye ameonyesha vipaji vya hali ya juu na anaichezea klabu ya Barcelona katika ligi kuu ya Hispania, La Liga.

Picha ya Mchezaji kinda Lamine Yamal (17) akiwa amebeba mtoto (3) ikisambaa na kudaiwa kuwa ni mtoto wake imetumiwa kwenye mitandao mbalimbali tazama hapa na hapa


Moja wapo ya taarifa zinazosambaa kuhusu Lamine Yamal na mtoto aliyembeba

Ufuatiliaji wa JamiiCheck katika vyanzo mbalimbali umebaini kuwa taarifa inayodai mtoto huyo ni wa Yamal haina ukweli. JamiiCheck imebaini mtoto huyo aliyebebwa anaitwa Keyne Yamal ambaye ni mdogo wa Lamine na sio mtoto wake kama inavyodaiwa.


Taarifa inayoeleza uhusiano wa Lamine Yamal na Keyne Yamal

Endelea kutembelea Jukwaa la JamiiCheck ili kuwa karibu na taarifa zilizohakikiwa
Sio mtoto wake ni mdgo wake
 
Huyo ni Mdogo wake...
 
Mnakimbilia kupost humu na hamjui kitu....huyo ni mdogo wake na siyo mtoto
 
Weka wimbo wa Africando au ule wa Afrika kuna mambo tuendelee kupata maneno kutoka studio zetu hapo Buzebazeba.🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…