Land Rover Discovery 4 - Ikoje hii gari, naomba uzoefu na ufafanuzi wake

Land Rover Discovery 4 - Ikoje hii gari, naomba uzoefu na ufafanuzi wake

Duksi

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Posts
229
Reaction score
576
Naihusudu sana Discovery 4 angalau kwa muonekano na chapa yake ya Land Rover, japo nikiri sijawahi kuiendesha hivyo siijui kivile.

Kama walivyo watu wengi wa ukanda wa Afrika Mashariki, tumekuwa tuikitumia magari ya mjapani haswa haya yaliochini ya kampuni iliyoanzishwa na Bwana Kiichiro Toyoda pamoja na ile kampuni ambayo mmoja wa mkurugenzi wake, Bwana Carlos Ghosn alitoroka kijasusi kutoka kuwa chini ya ulinzi mkali nchini Japan alipokuwa anakabiliwa na mshitaka mbali mbali ya ubadhirfu wa fedha na kukimbilia nchini Lebanon kupitia Uturuki. Aliziumbua mamlaka za kiusalama za kijapan zikibaki mdomo wazi ametorokaje tena kwa ndege.

Uzuri wa magari haya pendwa ya kijapan haswa Nissan na Toyota tunayamudu vizuri kutokana na ukweli kwamba vipuri vinapatikana kwa wingi na kwa bei himilika kuanzia vilivyotumia mpaka vipya. Vile vile magari haya ni imara na yanamudu barabara korofi za ukanda huu.

Sasa kama alivyowahi kusema bwana Maslow kwenye "Maslow’s Hierarchy of Needs", ukishatumia sana hizi gari zetu za kina sisi, unatamani kujaribu za juu kidogo (I am humbled).

maslow.jpg

Hivyo basi nimekuwa nikiitamani hii gari kutoka kwa Malkia Elizabeth II. Landover Discovery 4.

disc 1.jpg

dics 2.jpg

Gari hizi ni za Diesel, Automatic na ni CC 2,700 mpaka 3,000 na zimetengenezwa kuanzia mwaka 2009 mpak 2016. Bei zake pia zimechangamka kuanzia pound 10,000 kabla ya kusafirisha kwa UK na Japan naona CIF inaanzia $16,000 ukiweka Kodi bei inachangamka haswa, kodi yake inacheza kwenye shilingi mil 27 !

Mjini zipo nyingi tu vijana wanapush. Wajuzi wa haya magari hebu mtupe uzoefu wa hizi gari, je ni nzuri na madhubuti kwa matumizi ya mjini?

Changamoto zake, je ni gari nzuri Zaidi ya muonekano?
 
Hio kodi ya mil 27 umeipata wapi mkuu?

Kwny calc. Ya TRA disco.4 tena ya mwaka 2009 kodi yake ni 33mil na CIF yake waki estimate ni $12,947 sasa hio yako ya CIF 16,000 jiandae kwa kodi ya TRA kupanda maradufu.
 
Inategemea na mwaka, kwa mfano ya mwaka 2013, CIF ni $16,000 na kodi yake ni shs 25M.
👇👇
MV Calc.jpg
 
Back
Top Bottom