Hawezi kuacha kwa hali aliyofikia! Labda kwa msaada wa wafadhili kutoka nje. Kama huamini nenda pale Mikocheni A karibu na kanisa la TAG Samaria Church, kwenye soko kongwe na maarufu kama Gezaulole! Hapo ndipo anapolala uwani peupeee! Baada ya kutimuliwa na msamaria aliyekuwa akimsitiri chumbani mwake. Baadhi ya wasanii nguli wanachangia kuwa hivyo alivyo kwani huwa wanakuja hapo kinyemela na kumjulia hali na kumpatia vijihela kidogo naye huendeleza libeneke lake. Hali ya huyu dogo imekuwa mbaya nasema mbaya kama ninavyomjua kwa yakini. Na hii ni changamoto kwa wasanii wote wa kada zote katika sanaa kujikusanya na kuweka mkazo ktk suala la maslahi na ushirikiano wa dhati ili inapotokea mmoja wao amepata mushkeli ktk jema na baya waweze kusaidiana ktk msingi wa tatizo badala ya kumtembelea mwenzao na kumuachia vijihela bila kudili na mzizi wa tatizo alilonalo.