ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
WAKILISHA - SWANGILISH
Najiuliza hili swali sipati jibu kamili / Tunacho ongea wabongo kimombo Au kiswahili/ mkoloni katufilisi kiuchumi na kiakili/ anataka tufikiri tuna nuksi tusishamili/ ma Babu zetu walitekwa waliondoka wanalia/ siku hizi ukipata Visa ukiondoka unashangilia/ tuitunze lugha yetu ikipindi kungangamala/ tuhafiki mapinduzi kama "Guevara" / school masomo wange tafsiri kiswahili/ unafikiri watu wangefeli nakupata zefuri / nakueleza ukweli kiingereza hakina Dili/ tunakibeza kinashamili na kupoteza lugha Asili/ ukiongea kiswahili shuleni unatolewa mbele/ na shangaa lugha ngeni inavyopewa kipaumbele/ Mzungu anatuendesha utadhani wanasesere
/ tunarudishwa utumwani bila pingu wala kengele / shukurani kwa nyerere alicheza utadhani pele/ kuendeleza kiswahili mikoani na mbele mbele / unamfangilia mzungu sisi tunashinda tele/ kiingereza bila hela ni sawa na kupinga kelele...
( langa kileo a.k.a Raisi wa Gheto) - swanglish by wakilisha..
.
( katika picha ni mwana harakati Ernesto Che Guevara ambae marehem langa kileo katika wimbo huu wa SWANGILISH kutoka Crew ya wakilisha kamtaja)
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202