LATRA CCC yakusanya maoni ya matumizi ya Kadi za Mwendokasi, una lolote? Bonyeza Link utoe ya moyoni

LATRA CCC yakusanya maoni ya matumizi ya Kadi za Mwendokasi, una lolote? Bonyeza Link utoe ya moyoni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mamlaka ya Serikali ya Baraza la Ushauri Watumiaji Usafiri Ardhini - LATRA CCC (LATRA Consumer Consultative Council) imeanza kufanya utafiti na kuchukua maoni ya Wananchi na Wadau wengine kuhusu matumizi ya Kadi za Elekroniki zinazotumika katika usafiri wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka, Dar es Salaam (DART) maarufu kwa jina la Mwendokasi.

Ikumbukwe Septemba 2, 2024, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa alizindua kadi hizo na kusisitiza matumizi sahihi ili kusaidia kurahisisha huduma.
Licha ya uzinduzi huo baadhi ya Wadau wameonekana bado wakisuasua kutumia Kadi hizo katika huduma ya Mwendokasi, hivyo, upande wa LATRA CCC imeamua kukaribisha watumiaji wa usafiri huo kutoa maoni.

LATRA CCC imesema inapokea mtazamo wa Wadau juu ya matumizi ya Kadi ya Mwendokasi katika huduma za mabasi za BRT Jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya LATRA CCC imeeleza “Tunaomba utumie dakika chache kujaza fomu, maoni yako ni muhimu katika kuboresha huduma za usafiri ardhini. Tafadhali jaza fomu kupitia Link hii:

WhatsApp Image 2024-12-16 at 18.03.06_17f72edc.jpg

623667c6-4b29-49c8-b0ee-626bfec6e8b7.jpg

Ilivyokuwa siku ya Uzinduzi wa Kadi Septemba 2, 2024
Kabla ya uamuzi wa Serikali kisisitiza matumizi ya Kadi kwenye usadfiri huo, mara kadhaa Wadau wa JamiiForums.com waliwasilisha malalamiko yao kuhusu usumbufu wa matumizi ya fedha taslimu (cash) ambapo wengi wao walidai kuna changamoto ya utoaji 'chenji' kutoka kwa wahudumu, huku wengine wakidai Wahudumu wamekuwa na michezo ya upigaji kutokana na mfumo wa cash.

Kusoma Wadau zaidi kuhusu kero zao, bofya Link chini
~
Nakerwa na tabia ya wakata tiketi wa Mabasi ya Mwendokasi kudai hawana chenji kila siku

~ Mabasi ya Mwendokasi: Hili suala la mimi nakudai chenji wewe unanipa vocha ya VODA, kuna nini hapa?

~ Bila kadi sasa hupandi Mwendokasi. Waziri Mchengerwa awataka DART kutoa fursa Kwa Watanzania kuwekeza kwenye Mwendokasi

~ Wahudumu mabasi ya Mwendokasi wanatoza nauli zaidi ya iliyopangwa kwa kisingizio cha kukosa chenji

~ Serikali iamue moja; nauli ya Mwendokasi iwe Tsh. 700 kamili au 800
 
Je, maoni yetu yatafanyiwa kazi?

Abiria wengi hawatumii kadi kwa kuwa bado mamlaka ni kama zimefanya mfumo huo kama upo hatua za majaribio, hakuna ubunifu wa kutosha kuwahamasisha wananchi kutumia kadi.

Pia historia inawahukumu katika hilo kuna watu walipoteza fedha zao kwenye kadi za zamani
 
Waondoe kwanza wale wafanya kazi wao ..waliopo wana hasira sana kama hawalipwi .sasa mtu unachukua kazi ya nini kama una jijua sio mvumilivu
 
Binafsi sijaona maana ya kuweka hizo kadi kwakweli,
Kama kweli maoni yetu yatafanyiwa KAZI ondoeni tu hizo ndude.
 
Binafsi na wish sana kukutana na technical tema nina mawazo kadha kuhusiana na kuboresha huduma na kufanya iwe ya kisasa zaidi. Tu kumbuke lengo ni kutoa huduma na kurahisisha sio kukusanya pesa tu ila kumpa nafuu mtumiaji.
- Card iwe moja tu kwenye huduma za usafirishaji maanake; Kivuko, mwendokasi,daraja la nyerere, kwa mkapa, hata daladala kama vipi, mabasi ya mkoa. N card ni smart card inayo fanya kazi kwa mfumo wa NFC ilikuwa inaweza kuwa intergrated na system ya mwendokasi.
-Kutumia simu kufanya malipo; Hapa kuna njia mbili. kuna 1; App ya mwendokasi 2; Kwa kutumia Built in NFC system ya simu.
1; App ya mwendokasi. Hii ipo na ina weza tumika na mtu yeyote ila exposure yake kwa abiri bado ni ndogo. Hii natumia mara kwa mara na ina okoa mda sana. kwa sasa watanzania walio wengi wana miliki smartphone ila chaku shangaza utakuta mtu yupo busy na simu kwenye foleni ya mwendokasi akisubiri kununua ticket wakati uwezo wa kupata ticket kirahisi anao. So cha kufanya kuwe na mkazo au maelekezo watu wanunue ticket mtandaoni.
2; Matumizi ya NFC system ya simu. Hii pia ni mbadala wa kutembea na cards nyingi kwenye wallet na kutumia NFC ya simu direct. Hii ina tumika na nchi zilizo endelea kwa ajili ya huduma za subways etc, card zao nyingi au subways zao zina weza kuwa intergrated na simu kumpa urahisi mtumiaji kuweza tumia simu kama card kwaku touch au kuweka karibu na toll gate nayo kumpa huduma. Hii ita saidia kupunguza adha za kupoteza card au kununua kz walio wengi wanasmart phones hivyo ita kuwa rahisi kutumia simu kama card na kufanya walio wengi kutumia huduma kirahisi.

Mwisho ni hilo la kuweka Card moja kwenye mifumo yote ya kiserikali. Mlundikano wa card na kuweka pesa huku na huku na kumaintain zote ziwe na salio nayo ni changamoto ukizingatia kipato cha watanzania pia. Tunaomba hawa watoa huduma wote waletwe pamoja itoke card moja ya Taifa ihudumie kila kona ya nchi hii tena ikiwezekana hata iwe na nguvu kiasi cha kutumika kufanya manunuzi madukani na hata kuweka mafuta vituoni. Mfumo wa Ncard upewe nguvu ukuzwe uende zaidi na zaidi. Kesho kutwa uwanja wa Arusha una kamilika nao wata kuja na card zao?
 
Back
Top Bottom