Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) itaanza kuchukua hatua ya kutoza faini isiyopungua Shilingi 250,000 kwa daladala na mabasi ya mwendo wa haraka yatakayobebea abiria zaidi ya idadi iliyowekwa kuanzia wiki ijayo ili kuhakikisha hakuna msongamano katika vyombo hivyo.