KERO LATRA Dar na Pwani kusitisha vibali vya daladala za Mbezi kwenda Bagamoyo kwa madai zimepewa vibali kimakosa. Je, wamewatendea abiria haki?

KERO LATRA Dar na Pwani kusitisha vibali vya daladala za Mbezi kwenda Bagamoyo kwa madai zimepewa vibali kimakosa. Je, wamewatendea abiria haki?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na changamoto wakati wa kuhuisha leseni za LATRA Kwa waliopata mwaka 2023 ikidaiwa kuwa tumepewa kimakosa, huku tukifanya kazi kwa takribani miaka 2, Mwaka wa tatu huu unaambiwa umepewa kimakosa, Je, LATRA imewatendea haki wamiliki na Abiria wanaosafiri/kufanya shughuli katika njia hii ya MBEZI - BAGAMOYO?

Screenshot_20250210_194049.jpg

LATRA PWANI WAELEZEA
Jamii Forums
imewasiliana na Aisha Kuwa ambaye ni Afisa Mfawidhi LATRA Mkoa wa Pwani kuhusu hoja hii amesema:

“Kwa mkoa wangu wa Pwani hilo jambo halijafika kwangu, kwa kawaida wakikataliwa kupewa leseni huwa kuna maelekzo wanapewa, nadhani hilo ngoja tulifuatilie kwa ukaribu kujua kinachoendelea.”

Pia soma
~
LATRA Pwani: Tunaziwajibisha Daladala zinazokatisha ruti Mbezi - Mlandizi, pia tumesitisha utoaji wa Leseni mpya

~ LATRA Pwani na Dar mpo wapi? Daladala zinakatisha ruti Mbezi-Mlandizi zinaishia Njuweni MailiMoja!
 
Back
Top Bottom