ministrant
JF-Expert Member
- Jan 17, 2014
- 754
- 1,478
Kumekuwa na ukiukwaji mkubwa na wa wazi wazi wa maelekezo yenu juu ya bei elekezi za nauli katika njia hizo.
Watoa huduma wanatoza bei wanazotaka wao na kuwabighudhi abiria wanaotaka kulipa nauli elekezi.
Mathalani nauli kutoka Mbagala rangi 3 kwenda Kimanzichana ni Tshs. 3100/= lakini kwa makusudi kamili hutoza Tshs.4000/= bila kupepesa macho.
Hata mnapoleta Maafisa wenu katika njia hizi huishia kusimama tu barabarani bila kufanya ukaguzi yakinifu juu ya maumivi wanayopata wananchi katika viwango vya nauli.
Nashauri kiundwe kikosi kazi maalum kitakacho hakikisha nauli stahiki zinabandikwa ndani ya magari husika ili kuepusha ulaghai kwa wananchi.
Pia mkitaka kuyakamata magari hayo kwa uhakika, maafisa wenu waingie katika madaladala hayo na kujifanya wananchi wa kawaida walipe nauli mathalani ya kwenda kibiti waone viwango vinavyotozwa kama ni stahiki.
Imekuwa kero kubwa maana ujio wa maafisa wenu wanaoishia kusimama barabarani haujawahi kuwasaidia wananchi wa njia hizo dhidi ya udhalimu wa watoa huduma.
Nawasilisha.