LATRA na nyie pandisheni bei ili tufe kabisa

LATRA na nyie pandisheni bei ili tufe kabisa

zugimlole

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
2,078
Reaction score
1,352
Ndio hivyo tena
Ili TUFE vizuri kama wanavyotaka ili pia tusahau dipwedi Yao na akili iingie kichwani kwetu

Yaani kula itakua tabu kabisa kwani nyanya Moja tutanunua mia Tano Michele juu kabisa ufike bei ya kilo Moja kama urefu wa mlima Kilimanjaro na unga pia juu kabisa kuzidi mlima Everest

Ili TUFE hata Kwa msongo wa mawazo Kwa sababu tunanachonga sana na ni wajuaji sana

Tukomesheni TUFE tu hata Kwa mshituko wa moyo

EWURA MMEFANYA KAZI YENU VIZURI pongezi kwenu ila nadhani bahasha zilipita Kwa kuwapa wamiliki wa visima kuwa mafuta mnapandisha bei ndio maana jamaa wakaanza kuficha basi ikawa taabu sijui ni wiki mbili zile au Moja tu

Sijui tu yaani kiongozi wetu yupo kweli nikajua Mwijaku ni waziri naona anatoa matamko tu ya mama.

Dp imemficha kiongozi wetu anaogopa hata kuinua mdomo kutuliza Hali yupo kimya nadhani anaogopa kuambiwa analeta mipasho

Kazi ya kutuliza Hali na joto ni ya chawa tu

LATRA FANYENI KAZI YENU wamiliki wa vyombo vya usafiri mnawaumiza mafuta yapo juu na bei zipo palepale anzeni na mabasi ya daladala halafu mabasi ya mkoa malizieni na mwendokasi

LATRA mnasubiri nn?

MASOKO NA MAGENGE YOTE MITAANI hamuoni kinachoendelea hebu tukomesheni Na nyie bei zimepande


NADHARIA ZA KITAA
 
Back
Top Bottom