KERO LATRA Pwani na Dar mpo wapi? Daladala zinakatisha ruti Mbezi-Mlandizi zinaishia Njuweni MailiMoja!

KERO LATRA Pwani na Dar mpo wapi? Daladala zinakatisha ruti Mbezi-Mlandizi zinaishia Njuweni MailiMoja!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ujumbe huu uwafikie LATRA Pwani na Dar es Salaam nakala kwa wadau wote Serikali, Wasafiri, Wamiliki na UWAMADAR

Kwa ,uda mrefu sasa kumekuwa na Tabia ya Daladala zinazokwenda nje ya Dar es Salaam kutokea Kituo cha Mbezi Mwisho zenye ruti Mbezi-Mlandzi, Mbezi-Msata, Mbezi-Kwala na Mbezi-Mzenga kukatisha ruti inapofika mida ya jioni kuanzia saa kumi na moja na kuishia MailiMoja Njuweni.

Ombi kwa Wahusika wa LATRA wafuatilie suala hili na walikomeshe kwa mujibu wa Sheria za Nchi na LATRA maana linaleta usumbufu mkubwa kwa abiria hasa Wanawake Wazee na Watoto wanapoishia njiani na kulazimika kutumia pesa zaidi kufika sehemu wanazokwenda.

Ikishafika tu mida ya Saa moja usiku basi wahusika hao wanaanza visa, kwanza wanapandisha bei kisha ruti zinabadilishwa, matokeo yake ni kero kubwa hapo kituoni, Watu wanateseka.


Pia soma
~
LATRA Pwani: Tunaziwajibisha Daladala zinazokatisha ruti Mbezi - Mlandizi, pia tumesitisha utoaji wa Leseni mpya

~ LATRA Dar na Pwani kusitisha vibali vya daladala za Mbezi kwenda Bagamoyo kwa madai kuwa zimepewa vibali hivyo kimakosa. Je, wamewatendea abiria haki?
 
Back
Top Bottom