Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Februari 8, 2025, Mwanachama wa JamiiForums.com alitoa wito kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Dar na Pwani kushughulikia kero ya daladala zinazotoka nje ya Dar es Salaam, ruti Mbezi - Mlandizi kwa madai kuwa zinakatisha ruti na kuishia Njuweni Maili Moja.
Akasema kuwa hali hiyo inasababisha kero na kuwachelewesha abiria hasa majira ya jioni kwa kuwa wanakuwa wengi lakini daladala ni chache zinazoelekea Mlandizi.
Pia soma ~ LATRA Pwani na Dar mpo wapi? Daladala zinakatisha ruti Mbezi-Mlandizi zinaishia Njuweni MailiMoja!
LATRA PWANI WAELEZEA
Afisa Mfawidhi LATRA Mkoa wa Pwani, Aisha Kuwa amezungumza na JamiiForums kuelezea hatua zinazochukuliwa na pia ameweka wazi kwa sasa mamlaka hiyo imesitisha utoaji wa leseni mpya kwa baadhi ya ruti kutoka katika kituo hicho cha Mbezi.
Aisha Kuwa anasema “Tumekuwa tukiendelea na ukaguzi kuanzia asubuhi hadi jioni, hayo magari ambayo Mdau ameyalalamikia kuwa yanakatisha ruti sio tu Jioni hata mchana au asubuhi pia wapo wanaofanya hivyo.
“Tunashirikiana na Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wanaokiuka maelekezo ya leseni za huduma zao, tumeshatoa elimu sana lakini wapo wanaoendelea, ndio maana tumeamua kuwachukulia hatua.
“Pia ruti zote kuanzia za Mbezi kwenda Mlandizi, Mbezi – Kwala, Mbezi -Mzenga tumesitisha utoaji wa leseni mpya kwa kuwa inaonekana gari ni nyingi tofauti na idadi ya abiria ndio maana kuna muda hao wahusika wanasitisha ruti kwa kuwa wanaweza kuwa na abiria wachache, hivyo wanaona hasara kwenda nao hadi mwisho.
“Hakuna gari mpya inayoingia, ni zilezile zinazoingia zaidi ni wale wanakuuisha (renew).”