LATRA saidieni kurahisisha usajili siyo kutukwamisha

LATRA saidieni kurahisisha usajili siyo kutukwamisha

Somahiyo

New Member
Joined
Jan 17, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Habari wadau, mimi sio mwandishi mzuri ila ntajitahidi ili nieleweke.

Usajili wa gari za biashara hasa mpya ili zianze route imekuwa changamoto. LATRA wameweka vigezo ambovyo vingi vinawezekana ila kuna kigezo cha Dereva kufanya mtihani na hicho ndio changamoto.

Dereva anahitajika fufanya mtihani ili gari iweze kusajiliwa na kupewa route. Changamoto ni kufaulu mtihani, mtihani hauko open, dereva akifanya mwisho wa siku anatumiwa text kwenye simu, umepata alama 60, umefeli unahitajika kurudia mtihani.
  • Dereva amesoma NIT, ana cheti cha udereva bado anahitajika afanye mtihani wenu ili kusajili gari.
  • Kwa nini hii kazi msingewapa NIT wasimamie maswala ya mithani ya madereva nyie mkabaki kutoa leseni za usajili tu.
  • Madereva wanatuambia bila hela huwezi kufaulu mtihani, kwa hiyo mmetengeneza ka mradi ka kujinufaisha hapo LATRA na kutukwamisha biashara.
  • Wizara ya uchukuzi tunaomba muangalie hili, tunashindwa kusajili gari za biashara hadi upite njia za panya ndio upate usajili. Tusaidieni kwani hivi biashara ndio zinawaweka vijana wetu mjini na familia zao na sisi ndio zinatupa kuishi mjini. Watu wachache wasitukwamishe kupata mkate kwa tamaa zao.
  • Kitengo cha mitihani kitolewa LATRA wapewe NIT.
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom