LATRA simamieni maadili kwenye vyombo vya umma

LATRA simamieni maadili kwenye vyombo vya umma

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,883
Reaction score
14,600
Waslaaam Wahenga.

LATRA kama wadhibiti wa Mabasi na Daladala mnapaswa kulinda maadili ya jamii yetu.

Kumekuwepo na malalamiko ya Mabasi na Daladala kuonyesha picha zenye mahadhi ya ngono lakini hamtoi tamko lolote.

Ushahidi huu hapa daladala ya SIMU 2000 TO MNAZI T 292 ECX picha zake zinatia kinyaa.

Siitaji kusema sana lakini LATRA tunapaswa kuweka mstari katika hili.

1687761159414.png
 
Hili linaweza kukatazwa halafu baada ya siku mbili likapata uteteze kuwa kwa anayekereka abande basi lingine.

Ni kama ilivyokuwa kwa Miziki na makelele kwenye lilivyopata watetezi, likaja la waendesha mahubiri kwenye vituo vya daladala wakapata watetezi, ikaja ya machinga kupanga bidhaa barabarani likapata watetezi, likaja suala la mabasi yote kuingia Stand kuu ya Magufuli likapata watetezi na kusitishwa, likaja la TRA na wakwepa kodi wa Kariakoo nalo likapata utetezi likasitishwa

SIASA ZA NCHI HII NI NGUMU SANA
 
Mimi nina kesi na mabasi ya mkoa, mule ndani tunapanda watu tofautitofauti, washika dini na wapagani. Ajabu yake, kuanzia mwanzo hadi mwisho wanaweka picha za wapagani na wazinzi.

Ukitoka Dar kuanzia Kibaha hadi Norogoro utakutana na nyimbo za Diamond, Alikiba, Harmonize na mashetani mengine wakichezesha wanawake uchi na kutamka lugha chafu.

Toka hapo utakutana na Bongo Movie wanavaa vibaya ujinga mtupu. Basi wekeni hata nyimbo za dini kama ni Kaswida wekeni Kaswida na kama Kwaya wekeni Kwaya, mbona mabasi mengine yanaonekana kama ni ya watu wa dini sana lakini mnaendekeza kuhamasisha ngono?

Yaani ukifika mwisho wa safari nafsi imechafukwa kwa kulazimishwa kuangalia mapicha machafu machafu ya bongo flavour na bongo movie.

Chagueni za kuweka, ndani mule wengine tunapanda na wakwe, na mabinti zetu pia, hadi unaona aibu.
 
Hapo naona mdomo na risasi. Utuambie wewe unaona nini?

Tatizo wenda una mawazo fikra ya ngono kichwani mwako.
 
Tumia VAR mkuu
Papa fololo!!!!! Mnyama mkali sana mwacheni ameiheshimisha hii road ya mwenge mnazi!

Maudhui ya ngono yana shida gani mbona deep down mnapenda kudinyana afu huku kwa public mnazuga hamtaki!

Huenda jmaa hana maana hyo sema Kwa sababu we unapenda utelezi umepeleka mawazo yako huko haraka
 
Mimi nina kesi na mabasi ya mkoa, mule ndani tunapanda watu tofautitofauti, washika dini na wapagani. Ajabu yake,

Chagueni za kuweka, ndani mule wengine tunapanda na wakwe, na mabinti zetu pia, hadi unaona aibu.
Nunua gari lako tu.

Hizo nyimbo za dini wengine hawazipendi.
 
Papa fololo!!!!! Mnyama mkali sana mwacheni ameiheshimisha hii road ya mwenge mnazi!

Maudhui ya ngono yana shida gani mbona deep down mnapenda kudinyana afu huku kwa public mnazuga hamtaki!

Huenda jmaa hana maana hyo sema Kwa sababu we unapenda utelezi umepeleka mawazo yako huko haraka
Unafiki tu wa wabongo
 
mimi inakesa kwenye mabasi ya mkoa, mule ndani tunapanda watu tofautitofauti, washika dini na wapagani. ajabu yake, kuanzia mwanzo hadi mwisho wanaweka picha za wapagani na wazinzi. ukitoka dsm kuanzia kibaha hadi morogoro utakutana na nyimbo za diamond, alikiba, hamonize na mashetani mengine wakichezesha wanawake uchi na kutamka lugha chafu. toka hapo utakutana na bongo movie wanavaa vibaya ujinga mtupu. basi wekeni hata nyimbo za dini kama ni kaswida wekeni kaswida na kama kwaya wekeni kwaya, mbona mabasi mengine yanaonekana kama ni ya watu wa dini sana lakini mnaendekeza kuhamasisha ngono? yaani ukifika mwisho wa safari nafsi imechafukwa kwa kulazimishwa kuangalia mapicha machafu machafu ya bongo flavour na bongo movie. chagueni za kuweka, ndani mule wengine tunapanda na wakwe, na mabinti zetu pia.hadi unaona aibu.
Na zipo nyingine ni Injili Mbezi mpaka Nyegezi sisi wajukuu wa sheta mnatuonaje
 
😁😁Hv mtu muda wa kuangalia gari la mtu kulichunguza pande zote then ung'amue hlo! Kwa kwel watanzania tubinafsishwe kwa mwarabu
Hilo siyo gari la Mtu. Hilo ni gari la Umma na amelikatia leseni litumike kwa Umma kama chombo cha Usafiri. Kwa akili za hivi ndio maaana mnatetea Waarabu.
 
Hilo siyo gari la Mtu. Hilo ni gari la Umma na amelikatia leseni litumike kwa Umma kama chombo cha Usafiri. Kwa akili za hivi ndio maaana mnatetea Waarabu.
We ambae hutetei mwarabu umezuia waarabu kufanya nn?🤣
 
We ambae hutetei mwarabu umezuia waarabu kufanya nn?🤣
Mkuu mimi nilikua mstari wa Mbele kuandamana pale Mnazi Mmoja kupiga udhalimu. Wewe ulikua bizze kutafuta kula tunda kimasikhara
 
Mkuu mimi nilikua mstari wa Mbele kuandamana pale Mnazi Mmoja kupiga udhalimu. Wewe ulikua bizze kutafuta kula tunda kimasikhara
Mi nlikuwa baridi nawaangalia kwa dirishani kwenye Dala Dala saa mnasombwa
 
Acha kuona kla kitu ni ngono ukiona watu wanashikana unawaza ngono ukiona nguo fupi unawaza ngono iv ktk dunia ya leo ni movie au tamthilia gan hutoona watu wakishikana kuvutana kubusiana na ata kuvaa nguo fupi mavazi yasiyo na staha

Nazan wabongo mnahaja ya kuchange au kubadili mind set zenu dunia haijabadilika ila nyakati na watu wamebadilika maadili ayapimwi tena kwa mavazi mtu alovaa au msuko wa nywele mtu alivyosuka
 
Back
Top Bottom