KERO LATRA tumsaidie hili la Daladala kukatisha ruti Mbeya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) tunaomba mtusaidie katika hili maana sasa imekuwa mazoea Kwa madereva daladala.

Daladala za Nsalaga kwenda Stand kuu zimekuwa zinakatisha ruti kwa kuishia Mwanjelwa badala ya kufika Stand Kuu.

Ukiachana na hizo daladala za Nsalaga Kuna hizi za kutoka Mbalizi kwenda Uyole nazo mwendo ni uleule zenyewe zinaishia Kabwe hazifiki Uyole.

LATRA tunaomba liangalieni hili maana hii imekuwa kero kubwa sana kwa sisi Wananchi, utaratibu huu unaharibu sana ratiba zetu na ni usumbufu mkubwa.



 
Siku hizi hakuna SUMATRA Kuna LATRA mkuu
 
Ughwe! SUMATRA ili ku Indonesya kwa Kanji Laliji.
 
Ni Sumatra au Latra?

Unajua tz kuna organs nyingi sana na zingine hazijulikani ni za kazi gani.
 
Kwahiyo unataka ikiwa na mtu mmoja ipoteze mafuta kutoka kabwe hadi uyole
ACHA UFALA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…