Mwandishi Wetu, Dar es salaam
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka udhibiti Usafiri Ardhini, C.P.A, Habibu Suluo akiwa sambamba na Kamanda wa Trafiki, SACP, Ramadhan Ng'anzi, wameeleza kuwa kati ya Mabasi 759, yaliyokamatwa, Mabasi 723 yalipewa onyo na mengine 36 yamesitishiwa leseni zao.
Wakizungumza na Vyombo vya Habari wametolea ufafanuzi na kubainisha sababu ya Mabasi hayo kukamatwa, kufungiwa leseni na mengine kupewa onyo ni ukiukwaji wa sheria na kanuni za barabarani hali inayohatarisha usalama kwa abiria pamoja na mali zao.
Maamuzi hayo yanatokana na tathimini ya mamlaka ya usimamizi iliyofanywa na (LATRA), ikiwa imepita mwezi mmoja tangu Serikali iruhusu safari za Mabasi kwa saa 24, huku ikishuhudiwa ukiukwaji mkubwa wa sheria na kanuni za barabarani kwa baadhi ya makampuni.
Kutokana na ukiukwaji huo jumla ya mabasi 759, yalikamatwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kwa ushirikiano na kikosi kazi cha usalama barabarani, kwa makosa ya kuchezea mfumo wa VTS, unaodhibiti na kutoa taarifa za kasi ya gari pamoja na kudhibiti mwendokasi.
Suluona na Ng'anzi wamesema ''Mabasi yaliyositishiwa leseni kurejeshewa ni mpaka pale Mamlaka itakapojiridhisha kuwa wamebadilika ni 36, kati ya mabasi 246 ambayo ni sawa na asilimia 80, mabasi 1997 yamebainika yameendeshwa kwa mwendokasi kati ya km 86 hadi 89 kwa saa huku asilimia tisa yakiendeshwa kwa km 90 hadi 103 kwa saa''.
Wameendelea kwa kufafanua kuwa madereva 10, wamefungiwa kwa kuchezea mfumo tangu safari za masaa 24 kuanza octoba mwaka huu, lakini taarifa imeonyesha walioandikiwa faini kwa makosa ya mwendo kasi ni 666, waliofikishwa Mahakamani ni 32 na walioonywa ni 50.
Hata hivyo dereva atatakiwa kuomba kufunguliwa na ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani na kabla ya kufunguliwa atalazimika kutahiniwa ili kupimwa uwezo wake kwenye taaluma ya udereva, mara baada ya kumalizia kutumikia adhabu yake na ikiwa atafaulu atarejeshewa madaraja ya leseni yake kama atatetea sifa ya kuendelea kumiliki madaraja hayo.