LATRA yakanusha kuanzisha tozo za magari ya kubeba maiti. Yasema magari madogo yanayokodishwa ndio yatatozwa

LATRA yakanusha kuanzisha tozo za magari ya kubeba maiti. Yasema magari madogo yanayokodishwa ndio yatatozwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mamlaka ya usafiri ardhini LATRA imekanusha kuanzisha tozo kwa magari madogo ya kubeba maiti.

Mkurugenzi wa usafirishaji Kahatano amesema Serikali haijawahi kufikiria kuanzisha tozo ya namna hiyo bali mabasi madogo yanayokodishwa ndio yatatozwa tozo.

Mabasi madogo yenye uwezo wa kubeba abiria 14 hadi 30 ndio walengwa kwa sasa.

Chanzo: ITV habari

Pia soma > Magari yote ya kubeba maiti yatakiwa kulipa Tsh milioni

Maendeleo hayana vyama!
 
Ndio yale yale. Issue ni magari ya misiba kulipia kodi. Chezea vyote sio msiba; huko ni kwetu sote.

Busara ilikuwa kuondoa kabisa kodi pengine hata serikali ku- subsidize ili kupunguza kasi ya maeneo ya mijini kujaa makaburi.

Simple maths.
 
Juzi nilikuwa kwenye kikoa na latra kuhusu hilo sakata ni kama latra hawako tayari kushirikiana na wadau wa usafirishaji

Au huenda kiburi chao wanakipata kutoka kwenye mamlaka makubwa

Nani inamuingia akilini coaster ilipe gharama kubwa za vibali kuliko bus kubwa

There is so much more hawa majamaa ni kama huwa hawaend field kabla ya kuamua maamuzi yao
 
Hata mie nashangaa yani, harusi ndio haswa zilitakiwa zitozwe kodi. Ma MC wanapiga laki 7 mpaka million na nusu kila usiku. Kodi wanalipa wapi?
Tena wanaweza wasajili kwa annual fee na wakawapa efd machine kabisa....
Ukiacha MCs kuna
Mapambo
Picha
Magari said ya manne...
Sasa kwanin wasitozwe wao watoze misiba...
 
Tena wanaweza wasajili kwa annual fee na wakawapa efd machine kabisa....
Ukiacha MCs kuna
Mapambo
Picha
Magari said ya manne...
Sasa kwanin wasitozwe wao watoze misiba...
Yah harusi zina mapato makubwa sana ambayo serikali inayapoteza. Wakiwapiga laki 2 tu per event mara harusi zote kwa siku ni hela ndefu sana.
 
Juzi nilikuwa kwenye kikoa na latra kuhusu hilo sakata ni kama latra hawako tayari kushirikiana na wadau wa usafirishaji

Au huenda kiburi chao wanakipata kutoka kwenye mamlaka makubwa

Nani inamuingia akilini coaster ilipe gharama kubwa za vibali kuliko bus kubwa

There is so much more hawa majamaa ni kama huwa hawaend field kabla ya kuamua maamuzi yao
Halafu utawasikia eti mbona wadau wameshirikishwa!!!yaani wao kuongeza TAX BASE, inakwenda sambamba na viwango vya kukomoa watu!!badala ya kuweka kodi rafiki kwa mlipaji!!unadhani kwanini wazungu wao kukwepa kodi mtu anaona ni aibu kubwa sana, ni kutokana na kodi kuwa rafiki, vile vile anaona matumizi yake!!huku tunatiana ujinga eti kuwa mzalendo kwa kulipa kodi , kodi zenyewe hizo?!!unaongeza wafanya biashara 20, kuna wengine 50, wanafunga biashara!!!shida kubwa imeanzia kwenye mambo ya GAWIO, wote wamepewa kiwango cha kupeleka!!hujasikia TBS, nao kuanzia march, magari yote mapya watakagua wao!!kama halikidhi viwango unakwenda kulitengeneza kwanza, ndio wanalikagua!!!chaka jingine hilo!!!
 
Hii inatengenezwa iwe kama kikokotoo
Jambo hili litafikishwa bungeni keshokutwa litaleta malumbano marefu baadae Mkulu ataingiliakati atakuwa hero muda mwalimu tunzeni mtani tag
 
Back
Top Bottom