Nakushukuru ndugu hapo juu MASEETO, kwa jibu lako. Nisikuchoshe ama nisiwachoshe tu, nia ni kujua, maana naipenda sana kozi ya Sheria.
Kwa hiyo, wale waliofanya Bar Exam's, ilipoanzishwa hii Law School, walilazimika kwenda tena kusomea hiyo kozi ya Shule ya Sheria, ama kozi zinalingana tu na Bar Exam's, kimantiki hiyo?!
Nauliza hilo, maana kila aliyesomea sheria miaka hii, ili apate kazi (hasa Serikalini), na sasa lipo zaidi Sekta / Taasisi binafsi, lazima awe kasomea na Shule ya Sheria (Law School).
Natanguliza Shukurani Mkinijibu vema, lengo kuu nielewe. Nilipokosea mnirekebishe.
Ahsante!