Lawama hazijengi bali zinabomoa tu!

Mwanakijiji jibu unapopaswa kujibu,na Timing ni muhimu katika majibu yako...Lakini kumbuka pia si kila shutuma/Lawama inabidi uitolee maelezo...Kukaa kwako kimya kunaweza kuwa jibu zuri kuliko Maandishi.Kila unachoandika kinafika kwa wakusudiwa na wanaangalia Maandishi yako kwa macho yaliyovaa Darubini....

Kuna Wakuu walikuja kwenye Inauguration ya Obama,walichukua muda na kuzungumza nawe kwa kukupigia simu!!na ninaelezwa kuwa walikuwa wanataka kuonana nawe,lakini muda haukuwaruhusu,kuwa makini kwa kila anayetaka contact zako,adui huwezi kumjua kwa sura/maneno yake,wapo wengi humu...nafikiri "wameshindwa Hoja wanaleta vioja" Tupo pamoja nawe Mkuu,kazi yako tunaiona na tunaithamini.

Kijarida chako cha "cheche" nafikiri sasa kimekuwa Daily News,kwa sababu Waungwana walio wengi serikali wanakisoma ,Kiboreshe zaidi,kwani Jamii ya sasa inatambua kuwa Serikali ipo kwa ajili yao,na sio kama zamani ambapo Watawala walikuwa ni 'elites" fulani wasioguswa.Keep up Brother!!
 

Maneno mazito sana haya....usije ukaiweka wazi identity yako hata siku moja, niliisha wasikia wanene fulani wakiulizana namna ya kukupata na kukumaliza....zaidi nita kuPM....usiende Tanzania kijinga.

Masa
 

Kwa hakika Shy makala yako ni ndefu mno na nimeshindwa kuelewa unachomaanisha
 
Last edited:
Maneno mazito sana haya....usije ukaiweka wazi identity yako hata siku moja, niliisha wasikia wanene fulani wakiulizana namna ya kukupata na kukumaliza....zaidi nita kuPM....usiende Tanzania kijinga.

Masa

Mmhh...na wewe Nkwingwa sasa unaleta stori tu sasa....
 
Mwanakijiji ukiendelea kujibizana nao, nitashindwa kukuelewa. Achana nao please!

Hapa ndipo utakapogundua jinsi elimu yetu ilivyokosa ubora na jinsi isivyoandaa watu wetu. Baadhi yao ni viongozi hawa. Masikini Tanzania!

Nimewapata.... kwa kweli sikuwa na mpango wa kina wa kujibu kwani hilo jibu hapo juu linatosha tu. Kwa sababu mtu angesoma makala yangu ya j'tano nimemaliza kwa kuacha room ya kuendelea mapendekezo ya kujenga.

Mwawado, nimekupata vizuri tu, nazungumza nao wengi na ninafahamu si wote wana nia njema. Jambo moja hata hivyo nimejifunza ni kuwa adui ukimwogopa anapata kichwa. Mara zote niko makini lakini siongozwi na hofu. Tutajitahidi kuboresha na kuchagua mambo ya kufanya na kutolea maoni kuanzia sasa kwani kama usemavyo kuna watu wanapima tunachosema.

Thanks!
 

Mkuu I wish wangekuwa wanapima hayo maneno.Perhaps wangebadilika... Kwa sasa hawapimi, maana hatuoni tofauti.

Unajua sometimes, viongozi wetu they dont get it kabisa..! Wengi tunaopiga kelele its just out of love for our country. Nothing more. We refuse to allow people to think on our behalf! we refuse to see our fellow country men and women swimming in the ocean of poverty while few oligarchs are buying mansion in Dubai and Capetown. Worse, using tax payers money.

Tunasikitika mno, iweje..tuwe na wasomi waliotukuka, waliosoma shule nzuri kama viongozi wengine huko duniani..lakini sisi kila siku ndo kipimo cha UNDP na World Bank cha Umasikini? viongozi wetu wana TATIZO GANI? Tuna mkosi gani watanzania? Tusaidiwe vipi? Tumejaliwa kila kitu! Just name it. LAKINI kila siku umasikini ndo unaongezeka, viongozi wetu ni porojo tuu! Whyyyy??? Hawa jamaa hawana hata conscious jamani?????? Inauma!

Ukweli ni kwamba viongozi wetu wana frustrate sana, sana! Kuna vitu ungetegemea watu wavifanye hata kama wangekuwa na akili fupi kiasi gani! Mtu anapewa kazi lakini ni kuiba tuu...na aliyempa kazi..hamuwajibishi..

We jiulize kweli..Mtu kama Mkapa..na sheria zote zinazomlinda....ana uhakika wa pension nzuri mpaka kufa..lakini bado anawaibia wanachi masikini wa kutupwa! Tumfanyeje?? Honestly, sijui waafrika especially watanzania tulirogwa na nani! I dont know.

At times, watu kama Mwanakijiji nawaelewa....Mwanakijiji keep writing! Perhaps iko siku watasikia.
 
...........Hivi aliyeandika hiyo makala ni Shy?...............mbona naona watu wana-aim guns zao kwa Shy...........is this Shy obs.......?
 
Akili za kuandika utumbo kama alivyozowea mwanakijiji?
 
Inategemea unamaanisha nini na neno 'jadi'. Kiswahili ni lugha niliyojifunza na ninayoendelea kujifunza.

Basi naomba katika kujifunza kwako, tamka zo e a halafu tamka zo we a halafu utapata lipi ni sahihi.

Kwa upande wangu, Ki-swahili, ni lugha ya jadi, nimezaliwa, nimekulia, na nimesoma, u-swahilini. Dar Es Salaam, pwaniiii, kwenye chipuko la ki-swahili
 

Mkuu sitokupinga kuhusiana na kujua kwako lugha ya Kiswahili. Sababu ninayoweza kuipinga ni ile inayoashiria uthibitisho wa hilo, kama nilivyoainisha kwa wekundu; ninaipinga kwa asilimia kadhaa kwa kutumia mfano huu: Je, hujawahi kusikia watu ambao hawakuzaliwa Marekani au Uingereza na kukulia huko wakiongea na kuandika Kiingereza fasaha kuliko wazawa na waliosomea au kukulia huko?!
 

Yawezekana tena sana, lakini kwa hili la mazoea na mazowea, bado hujaniridhisha.
 
Mmhh...na wewe Nkwingwa sasa unaleta stori tu sasa....

Nyani, upo? Yaani unaniacha hoi na hizo avatar zako yaani tangu mwishoni mwa mwaka jana hadi sasa umebadilisha mara 3!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…