Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
Wakati Wazungu ndo wamemalizia Berlin Conference (1884-85), Mwezi huo wa Februari, Chancellor Otto von Bismarck wa Ujerumani alitangaza barani Ulaya kuwa, Eneo lote ambalo Carl Peters alifanya Mikataba (ya kilaghai) na Chief Mangungo wa Msovero (Morogoro), liko chini ya Himaya (Possession) ya Ujerumani. Maana yake eneo lote kuanzia Morogoro hadi Pwani liliwekwa chini ya Ujerumani, japokuwa Sultan Barghash bin Said alipinga ila alikubali baada ya Wajerumani kupeleka meli ya kivita kumtishia ndipo Waingereza waliingilia kumsaidia na kufikia Anglo-German Agreement ya 1886, iliyompa Sultan Maili 12 za Pwani kutoka Mto Ruvuma hadi Kisimayu (Somalia).
Wajerumani (DOAG) walipoanza kutoza kodi katika maeneo ya Pwani, wafanyabiashara walipinga na kusababisha Vita ya kwanza iliyoongozwa na Abushir Bin Salim (1888-89) huko Pangani. Lakini ilisubiriwa mpaka 1890 wakati Serikali Ujerumani ilipochukua uendeshaji kutoka DOAG na kumteua Gavana Julius von Soden, ndipo mapambano hasa ya interior yalipoanza hasa vita vikali ya Mtwa Mkwawa (Lugalo) mwaka 1891 baada ya Mkwawa kuwataka watoe hongo kwenye Njia ya kwenda mikoa ya ndani. Wajerumani walimshinda mwaka 1894 huko kwenye ngome yake ya Kalenga. Wengine waliopigana kishujaa sana ni: Mtemi Isike wa Unyanyembe 1893 na Mangi Meli wa uchagani. Wengine waliojitahidi ni Wangoni, Wayao (Machemba), Ujiji (Tagaralla), but majority ya Watanzania wali-succumb kwa Wajerumani kutokana na nguvu walizoonyesha kuwa nazo.
Lakini cha ajabu ni kuwa, Wamasai na Waberbaig ndiyo makabila ambayo yamekuwa yakihofiwa sana kwa ukali na ushujaa kuanzia kwa Wasukuma, Wanyilamba, Wanyaturu, Waisanzu, Warangi, Wasandawe, Waalagwa, Wagorowa, Wambulu, Wambugu, Wakaguru, Wanguru, Wazigua, Wasambaa, Wapare, Wachagga hadi kwa Wameru. Lakini hayakufanya chochote cha maana cha kupigana na Wajerumani.
Hao Wakurya, nao ni mashujaa sana kwenye siasa nchini kwa kutoogopa na kujiamini. Nilipokuwa UDSM, nilishangaa kuona aliyeshinda Urais alikuwa Mkurya, kufuatilia nikaambiwa hata wawili waliopita nao walikuwa Wakurya.
Indeed Watanzania wengi wanawaheshimu sana kwa jinsi walivyomlilia sana Nyerere na kulazimisha kutoa Volunteers wa kushiriki Vita ya Kagera 1978-79. Kila Mkoa ulipaswa kutoa askari 2000 but Mkoa wa Mara ulilalamika kuwa, ratio hiyo ni ndogo sana kwao. Kulitokea mgogoro mkubwa juu ya idadi hiyo ndipo walipoingezewa hadi 4,000 though inaonekana walizidi hiyo pia kwani inaelezwa Mikoa mingine hata 1000 hawakufika.
Walikuwa wapi enzi za kunyanyaswa na Wajerumani? Mbona hawakufanya chochote cha maana wasitawaliwe?