Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa sasa.
Nimefuatilia sana lawama zinazotolewa kwa viongozi mbali mbali wa nchi yetu Tanzania.
Kinachonipa wasi wasi ni kuona kuwa lawama hizo zinaelekezwa tu kwa wale viongozi ambao ni wana CCM.
Najiuliza haya:-
1. Ni kweli kwamba hakuna la maana wanalilifanya viongozi wana- ccm?
2. Je viongozi, Wabunge, nk. wa Itikadi nyingine za siasa hwana lawama?
Wako safi tu?
3. Viongozi wa taifa letu hawana lolote la kusifiwa?
Mbona lawama ndo nyingi zaidi? Na ni kwa wana- CCM tu?
Mimi nashauri mema yasemwe na mabaya pia .
Yasemwe hayo mema na mabaya bila kujali itikadi ya siasa ya mhusika.
Nini msingi wa maswali yako (nini kimekusukuma kuuliza)? maswali yako ni ya kijiweni mno, yamekosa pa kujishika. Nashindwa niandike vipi ili upate kunielewa.
Maybe ujiulize mwenyewe maswali yafuatayo:-
(1) Je viongozi wana CCM wanambiwa hakuna la maana wanalofanya.
Mimi nimeona na kusikia mengi mazuri hata hapa JF zipo thread hizo.
(2) Je viongozi wa vyama vingine vya siasa hawalaumiwi?
Mimi naona lawama nyingi tu kwa akina Lipumba, Mbowe, Zitto nk
(3) Je viongozi wa Taifa letu hawasifiwi kwa yale wanayotenda?
Mimi naona sifa nyingi tu zikitolewa kwenye media na forums mbalimbali
Suala la lawama kuwa nyingi kuliko sifa, ni rahisi kulijibu. Mosi ni kwasababu kero zimezidi. Kumbuka CCM ndo imeshika dola. Sasa wewe ulitaka wananchi wazipeleke wapi kero na lawama zao. Hakika nimeshindwa kukuelewa kabisa.
Unashauri mema yasemwe na mabaya pia. Kwani sasa ipoje? wewe unataka mema na mabaya tasemwe kwa kiwango sawa, Je, kwa kipimo kipi? Pole sana mkuu poor questioning. Otherwise u-substantiate wapi unakoongelea (kwenye media, JF au wapi?) kama ni general ...