Lawama sita kwa Sitta

Lawama sita kwa Sitta

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Kwanza, namlaumu kwa kukiuka Kanuni za Bunge Maalum la Katiba ambazo zinataka Rais Kikwete aanze kulizindua Bunge hilo kabla ya Jaji Joseph Sinde Warioba kuwasilisha Bungeni humo Rasimu ya pili ya Katiba kwa Mjadala.

Pili, namlaumu Mh.Sitta kwa kupanga ratiba za Bunge Maalum la Katiba kama ni shughuli zake binafsi.Rtiba za Bunge hilo ni kwa mujibu wa Kanuni za Bunge hilo na si vinginevyo

Tatu, namlaumu Mh.Sitta kwa kumsumbua Jaji Warioba hadi Dodoma na baadaye Bungeni alikoshuhudia kelele,zomeazomea na mayowe

Nne, namlaumu Mh.Sitta kwa kutaka kutumia cheo chake bila ya kuzingatia Kanuni ambazo ndizo hasa zinazompa mamlaka yake na mipaka ya mamlaka hayo

Tano,namlaumu Mh.Sitta kwa kusababisha Bunge Maalum la Katiba kuonekana kituko.Walichokifanya Wajumbe ni kuonyesha kutokubaliana na ratiba ya kuanza Jaji Warioba kabla ya Rais Kikwete

Sita, namlaumu Mh.Sitta kwa kukiuka Sheria ya Marejeo ya Katiba,2011 kifungu cha 24 (5) kwa kuanza shughuli za Bunge Maalum kabla ya kuapishwa kwa Katibu na Katibu Msaidizi wa Bunge hilo. Hawa wanapaswa kuapishwa na Rais Kikwete.Bila hawa hakuna Bunge na shughuli haziwezi kuanza. Mantiki ni kwamba Rais awaapishe na kuzindua Bunge kwanza.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete awaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Leo Mjini Dodoma. ~ JIACHIE

Rais Kikwete amwapisha Katibu wa Bunge Maalum na Naibu wake - YouTube
 
Petro suala la kuapishwa makatibu kubali kuwa umechemka,unataka kulazamisha kuapishwa kuendane na uzinduzi
 
Mimi niwape Shikamoooooooooooooooo!! WABUNGE waliokataa ubabe wa Sitta na mipango ya chini ya kitanda ya Maccm. Lengo lao ni kutaka kupuuza maoni ya wananchi. Nimeshangaa sana eti wanasema Rais amebanwa na shughuli zingine.. hivi ni shughuli gani ambazo ni nyetii mpaka zimbane Rais kushindwa kuzindua Bunge?? Hapo angesikia msiba wa msanii hata kama ni Kigoma angeacha shughuli za Serikali na kwenda msibani....

Mipango yao imeshagundulika, Wanataka Warioba aanze ili JK aje kujibu kwa kutoa maelekezo... Haikubaliki hiyo. JK azindue ndipo Jaji Warioba apewe muda wa kutosha kuwasilisha maoni yetu wananchi, tena wasimdhalilishe, yale maoni ni ya kwetu sisi...

Hii nchi si ya CCM peke yao.. nchi hii ni ya kwetu sote..

Nasema SHIKAMOOOOOO WABUNGE kwa kukataa kuburuzwa na hiyo ndiyo iwe njia ya kukataa kuburuzwa... shenziiii!!!
 
Sita ameanza kazi vibaya anaanza kuonyesha amecompromise na kuungna na kina Chenge kuhujumu katiba mpya.
 
Huyu sitta mbona anataka kujiumbua badala ya kujenga heshma? Ila tumpe muda
 
Mbona juzi tuu hapa mlikuwa mnamfagilia?
 
Mimi niwape Shikamoooooooooooooooo!! WABUNGE waliokataa ubabe wa Sitta na mipango ya chini ya kitanda ya Maccm. Lengo lao ni kutaka kupuuza maoni ya wananchi. Nimeshangaa sana eti wanasema Rais amebanwa na shughuli zingine.. hivi ni shughuli gani ambazo ni nyetii mpaka zimbane Rais kushindwa kuzindua Bunge?? Hapo angesikia msiba wa msanii hata kama ni Kigoma angeacha shughuli za Serikali na kwenda msibani....

Mipango yao imeshagundulika, Wanataka Warioba aanze ili JK aje kujibu kwa kutoa maelekezo... Haikubaliki hiyo. JK azindue ndipo Jaji Warioba apewe muda wa kutosha kuwasilisha maoni yetu wananchi, tena wasimdhalilishe, yale maoni ni ya kwetu sisi...

Hii nchi si ya CCM peke yao.. nchi hii ni ya kwetu sote..

Nasema SHIKAMOOOOOO WABUNGE kwa kukataa kuburuzwa na hiyo ndiyo iwe njia ya kukataa kuburuzwa... shenziiii!!!

yeye atoe hotuba yake aafu asepe atuachie warioba wetu.wakenya nao watimke kabla hatujawa do
 
Back
Top Bottom