Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Kwanza, namlaumu kwa kukiuka Kanuni za Bunge Maalum la Katiba ambazo zinataka Rais Kikwete aanze kulizindua Bunge hilo kabla ya Jaji Joseph Sinde Warioba kuwasilisha Bungeni humo Rasimu ya pili ya Katiba kwa Mjadala.
Pili, namlaumu Mh.Sitta kwa kupanga ratiba za Bunge Maalum la Katiba kama ni shughuli zake binafsi.Rtiba za Bunge hilo ni kwa mujibu wa Kanuni za Bunge hilo na si vinginevyo
Tatu, namlaumu Mh.Sitta kwa kumsumbua Jaji Warioba hadi Dodoma na baadaye Bungeni alikoshuhudia kelele,zomeazomea na mayowe
Nne, namlaumu Mh.Sitta kwa kutaka kutumia cheo chake bila ya kuzingatia Kanuni ambazo ndizo hasa zinazompa mamlaka yake na mipaka ya mamlaka hayo
Tano,namlaumu Mh.Sitta kwa kusababisha Bunge Maalum la Katiba kuonekana kituko.Walichokifanya Wajumbe ni kuonyesha kutokubaliana na ratiba ya kuanza Jaji Warioba kabla ya Rais Kikwete
Sita, namlaumu Mh.Sitta kwa kukiuka Sheria ya Marejeo ya Katiba,2011 kifungu cha 24 (5) kwa kuanza shughuli za Bunge Maalum kabla ya kuapishwa kwa Katibu na Katibu Msaidizi wa Bunge hilo. Hawa wanapaswa kuapishwa na Rais Kikwete.Bila hawa hakuna Bunge na shughuli haziwezi kuanza. Mantiki ni kwamba Rais awaapishe na kuzindua Bunge kwanza.