Lawama zote kwa sasa Serikali isizikwepe na inapaswa kulaumiwa kwa kila kinachoendelea/kitakachoendelea!

Lawama zote kwa sasa Serikali isizikwepe na inapaswa kulaumiwa kwa kila kinachoendelea/kitakachoendelea!

Paulsylvester

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2021
Posts
1,464
Reaction score
3,379
Majuzi juzi wabunge walikuwa wanashangaa ndoa kuvunjika kwa wingi kwa muda mfupi na wanaume wengi kukimbia ndoa zao,

Lakini hawajiulizi ni kwa nini inakuwa hivi,

Dume kama Dume, kawaida yetu sisi, tumeumbwa ili tule kwa jasho na kuhakikisha familia inaishi kwa furaha bila tatizo lolote la njaa, na Dume kama Dume, huwa haliko tayari lichekwe na majirani kisa watoto wa lenyewe wanalala njaa, hiyo huwa hatuwezi aisee, hapo mwanaume wa shoka atapambana kwa jasho na damu

Mambo yanspokuwa magumu zaidi, kikawaida Dume kama Dume, huwa linaamua kupeleleza ni wapi ambako linaweza kwenda pesa chapchap

Likishapata, liraiaga vema familia na kisha safari, sasa huko ni mawili, kwanza, litaondoka likiwa linajua hali ni mbaya saana home, likishafika huko, mambo yasipokwenda kama lilivyotarajia, huwa ni vigumu saana kurudi kwa familia

Wanaume sisi, huwa hatuko tayari kuona mateso ya familia zetu, eti siku mbili nyumbani hakuna msosi? Hapo nimekopa kwa mangi mpaka mangi akiniona tu anaondoka dukani kwake!

Katika hali ya kawaida, wanaume sisi si watu tusiopenda fedheha, ila mambo yanatulazimisha tuu

Hoja ni kwamba, Serikali inapswa kutwishwa lawama zote na migogoro yote inayoendelea sasa, kwa sababu,

Kwanza viongozi wetu, mpaka sasa, hawajui ikiwa zipo familia zinalala njaa,

Viongozi wetu mpaka huu muda, hawajui kabisa hali ngumu wanayopitia wananchi wao, kwa sababu, hakuna walichojinyima, kama ruti za nje ndio kwaaanza zinazidi kuja, kama posho, ndio kwanza kila kukicha wanabuni mbinu ya kujiongezea posho, mishahara mikubwa, kuagiza magari ya kifahari

Hawaingii dukani kwa mangi kujua uhalisia wa bei, kila wanachotaka kinaagizwa tu, kiukweli wanaishi utazani hawataki tena peponi, wakati mwingine wanajiuliza, peponi ni pazuri kama wanavyoishi sasa?

Jamani, sielewi kwa nini viongozi wetu hawana huruma,

Matatizo ya wananchi kwa sasa ni mengi, na hata hao panya road, kama kungekuwa na unafuu wa maisha unadhani wangeliipenda hiyo kazi ya hatari kiasi hiko, wanachapwa lisasi na kuuwawa, unadhani wanataka?

Na hiyo hali ngumu ya maisha, ikiwa sugu sana, kuna hatari ya watu kujiingiza kwenye ujambazi sugu na hata ugaidi ili tu waweze kukidhi mahitaji yao

Lakini ni Nani atalaumiwa? Ndiyo ni wao wakulaumiwa, lakini ni nini chanzo?

Mnadhani kwamba hiyo ni roho? Au wanasababishiwa..?

Serikali inayojali wananchi wake, hauwezi ikakaa kimya tu na kuacha mambo yajiendee tu bila udhibiti wa vitu mhimu

Ugumu wa maisha, serikali haiwezi kukwepa lawama!

Viongozi wanajua kabisa kwamba, hali ni tete, wanatutwisha tozo? Ili iweje sasa, mbona wao hawachi kuagizwa vya anasa.?

Wanaume wa TZ kwa sasa, tunapitia hali ngumu kiasi cha wengi kuwa na vichaa!

Kuwa kichaa si wakati wote kwamba mtu umeugua, no, wamati .wingine mambo yanapokuwa Tait sana

Mtu mwingine aweza kusema nalalamika ili hali nazungumza kwa kukelwa na jinsi ambavyo viongozi wetu hawajali maisha ya wananchi

Na mhimu kuwaambia
 
Mahindi sado 4500
Mchele kilo 3000
Bando hazishikiki
Ajira hakuna
Umeme unakata mda wowote
Kila kitu kimepanda bei

Hakuna wa kumsaidia masikini, serikali haipo kwa ajili ya masikini.

Dua la kuku halimpati mwewe
 
Back
Top Bottom