Hiyo ni kwa sababu ya inflation. Ili uchumi wa nchi uonekane una afya inabidi uwe na ka inflation ka do go au ka inflation kwa mbali, kama vile chumvi kwenye mboga. Ina maana kama mia tano leo inanunua maandazi matano basi mwaka kesho hiyo hiyo mia tano inunue maandazi manne. basi ukienda hivyo kwa muda wa miaka kama mia mbele utakuta elfu tano ndo unaweza pata maandazi matano. Hivyo kupelekea elfu tano note iwekwe katika sarafu kwasababu ya kuwa na mzunguko mkubwa hivyo kuwa katika form ya sarafu haitachakaa kama note.