Uchaguzi 2020 Lazaro Nyalandu ni mgombea bora mara 100 ya Membe

Uchaguzi 2020 Lazaro Nyalandu ni mgombea bora mara 100 ya Membe

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Membe anakuja upinzani baada ya kubwagwa 2015. Watu wa aina hii wakikarihishwa juice za chamwino hawakawii kusujudia minazi ya chamwino

Lazaro Nyalandu anajua nini anafanya na hana papara. CHADEMA kama chama makini naamini Lazaro Nyalandu anaweza kukiweka chama kwenye ramani kuliko huyu aliye katwa mkia

FB_IMG_1594991803947.jpeg
 
Nazidi kupata hofu na ajenda ya ACT wazalendo, kinaweza kuwa kifo cha siasa za Maalim Seif, ni kama kilibuniwa ili kuwa neutralize wapinzani tishio kwa dola.

Wapinzani wa kweli wawe makini.
 
Mimi naona ni sawa ccm imewakopesha wapinzani,hapa ndoo nakikubali chama cha CCM,hii ni aibu kwa upinzani,membe ni CCM,nyarandu ni CCM na makufuli ni CCM,miaka 25 wapinzani hawajajiandaa kuandaa watu wao? yaani wasio kuwa na thamani CCM wakija upinzani ndoo wenye thamani,
 
Katika viongozi wasio na ushawishi walio ondoka ccm namba moja ni membe. Ana hasira.. watabomoa hata zile hoteli zake kule mtwara.
Tulieni mnyolewe. 2020 twende na Membe, ndo amekuja Sasa hebu nendeni naye acheni kulia lia!
 
Ni kweli maana Membe amekuja kwasababu ya Urais pekee
 
Membe ni mgombea wa ACT,labda utuambie Nyalandu ni bora kuliko Lisu hapo utaeleweka.
Membe agekuwa asset kwa upinzani iwapo angesema kuwa ninaondoka CCM kwa vile sijaridhishwa na mambo yanayofanywa na serikali; hivyo, ninakuja huko ili kujenga nguvu. Lakini asubiri asurubiwe na CCM ndiyo akimbilie upinzani, sioni kesho yake yenye maana. Afadhali na Lowasa alikuwa imewekeza muda kwa wafuasi wake lakini sio huyu tuliemsikia jana kuwa ana wafuasi maelfu nyuma yake!
 
Sasa hapo unataka ACT wafanyeje,maana wao wamemuona kwao ni mtaji, kuliko wagombea wengine kwenye chama chao.
 
Mambo mengine hayahitaji akili kubwa sana. CCM ilizaliwa 1977 kutokana na TANU ambayo ilizaliwa 1954. Vyama vya upinzani vilianza kuzaliwa 1992. ACT imezaliwa 2014/15. Hao ambao hawajahi kupita CCM watatoka wapi. Ama unataka watoto waliozaliwa kuanzia 1992 ndio peke yao wawe upinzani? ACT ikikataa waliotoka vyama vingine, itabakiwa na watoto wenye miaka 5-6 tu - waliozaliwa wakati inaundwa!!
Mimi naona ni sawa ccm imewakopesha wapinzani,hapa ndoo nakikubali chama cha CCM,hii ni aibu kwa upinzani,membe ni CCM,nyarandu ni CCM na makufuli ni CCM,miaka 25 wapinzani hawajajiandaa kuandaa watu wao? yaani wasio kuwa na thamani CCM wakija upinzani ndoo wenye thamani,
 
CCM A

CCM B

CCM C

bora nichague ccm A kuliko B na C zilizojivika upinzani feki
 
Tunaweka kumbukumbu sawa Nyallandu alikuwa miongoni mwa waliochukua form kuomba ridhaa ya kugombea Urais kupitia CCM. Wewe sema tu CHADEMA ndiyo isimamishe mgombea Uraisi na vyama vingine vimuunge mkono mgombea wa CHADEMA kama ilivyokuwa 2015 kwa sababu ndiyo kwenye haki zaidi.

Hata ikisimamishwa Zitto utasema Nyallandu ni bora kuliko Zitto, ni haki yako kwa sababu unapigania chama chako CHADEMA.
 
Utasikia hotel yake ipo kwenye road reseve
Membe agekuwa asset kwa upinzani iwapo angesema kuwa ninaondoka CCM kwa vile sijaridhishwa na mambo yanayofanywa na serikali; hivyo, ninakuja huko ili kujenga nguvu. Lakini asubiri asurubiwe na CCM ndiyo akimbilie upinzani, sioni kesho yake yenye maana. Afadhali na Lowasa alikuwa imewekeza muda kwa wafuasi wake lakini sio huyu tuliemsikia jana kuwa ana wafuasi maelfu nyuma yake!
 
Ukweli Nyalandu amenifurahisha sana pia. nina uhakika akirudi kwenye Ubunge hakosi na atafanya vizuri zaidi kuwa mkosoaji wa Serikali hii. URais ampgie tu debe ndugu yake Tundu Lissu!
 
Member alishampinga huyu toka 2015 na kimsingi Nyalandu hana uhodari na ujasiri kama alionao Membe!! Eti polipoli anashiriki kumtimua Membe kweli,huyo bushir anaanzaje kumhoji Membe!! Acha aje upinzani
 
Nazidi kupata hofu na ajenda ya ACT wazalendo, kinaweza kuwa kifo cha siasa za Maalim Seif, ni kama kilibuniwa ili kuwa neutralize wapinzani tishio kwa dola.

Wapinzani wa kweli wawe makini.
Hakuna kitu kama icho kitu ni coincidence hakuna aliyepanga wala kubuni.
 
Back
Top Bottom