Lazima ujue kutofautisha hivi vitu kingereza ni lugha nyepesi sana, jifunze kitu hapa

Lazima ujue kutofautisha hivi vitu kingereza ni lugha nyepesi sana, jifunze kitu hapa

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
IPI TOFAUTI KATI YA “COME BACK” NA “GO BACK”?

Kwenye post hii, naenda kukupa tofauti kati ya “come back” na “go back”.

Maneno yote mawili “Come back” na “go back” humaanisha “rudi” au “kurudi”.

Mfano unaposema “come back home” unamaanisha ‘rudi nyumbani’, na ukisema “go back home” pia unamaanisha “rudi nyumbani”.

JE, TOFAUTI IKO WAPI KATI YA “COME BACK” NA “GO BACK”?

1. Come back
‘Come back’ humaanisha ondoka na rudi hapa katika eneo ulilopo wakati unazungumza. Chukulia una safari ya nje ya nchi, bado upo Tanzania, na unasema utarudi, basi katika mkutadha huu unaweza kusema “come back”. Mfano: “I will come back” – Nitarudi.

TUTAZAME MIFANO:
SITUATION #1: Ms. Romana talks to his teacher, Mr. Wilson (Romana anaongea na mwalimu wake, Wilson)

Romana: “Excuse me, Mr. Wilson. I need to leave, but I'll come back in 15 minutes. (Samahani, Wilson. Nahitaji kuondoka, lakini nitarudi ndani ya dakika 15)

Mr. Wilson: It’s okay, Ms. Romana!(Ni sawa, Romana)

SITUATION #2: An angry mother talks to his Son (Mama mwenye hasira akiongea na kijana wake)

Mother: Get out of my house and don't come back! (Ondoka nyumbani kwangu/kwenye nyumba yangu na usirudi)

Son: Forgive me, mom! I won’t do it again! (Nisamehe mama! Sitarudia tena!)

SITUATION #3: Msafiri Visits Mtaalamu wa Kiingereza Office (Msafiri anatembelea ofisi ya Mtaalamu wa Kiingereza)

Msafiri: Good morning, madam! (Habari za asubuhi, madam!)

Secretary: Morning!. How may I help you? (Nzuri! Nikusaidieje?)

Msafiri: I’m looking for Mr. Wilson. May I see him? (Namtafuta Wilson. Naweza kumuona?)

Secretary: I'm sorry, he isn't here. But he's coming back tomorrow. (Samahani, hayupo hapa. Lakini anarudi kesho)

2. Go back
‘Go back’ humaanisha rudi kule ulipokuwa mwanzo au ulipotoka. Unakuwa unaongea hivi ukiwa ugenini au sehemu uliyotembelea. Mfano (wewe mtanzania) umetembelea Marekani, na unataka kusema utarudi Tanzania, basi unaweza kutumia ‘go back’ katika muktadha huu. Mathalani unasema “I will go back to Tanzania next month” – Nitarudi Tanzania mwezi ujao.

TUTAZAME MIFANO:
SITUATION #1: Wilson talks to his lovely wife (Wilson anaongea na mke wake kipenzi)

Mr. Wilson: “I don’t have really much time to stay here, I have to go back to my office”. (Sina muda mwingi wa kukaa hapa, Inabidi/natakiwa nirudi ofisini kwangu)

Wilson’s wife: “Really honey! When will you go back? (Kweli kipenzi! Utarudi saa ngapi?)

SITUATION #2: Boudia talks to Mr. Mood after a short visit (Boudia anaongea na Mood baada ya kumtembelea/ ziara fupi)

Boudia: I've had a lovely time, but I should go back home now. (Nimekuwa na wakati mzuri, lakini ninapaswa kwenda nyumbani sasa)

Mood: “Stop kidding, buddy! Why are you in a hurry?” (Acha utani, rafiki! Kwanini una haraka?/ mbona haraka?)
 
IPI TOFAUTI KATI YA “COME BACK” NA “GO BACK”?

Kwenye post hii, naenda kukupa tofauti kati ya “come back” na “go back”...
To make a long story short ni kwamba..

Go back : rudi huko,rudi kule.

Come back : rudi hapa,urudi hapa.

NB : HAPA ni sehemu ambayo mazungumzo yanafanyika.
 
Back
Top Bottom