Lazima utakuwa umeonewa kama.......

Lazima utakuwa umeonewa kama.......

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
UTAJUAJE KAMA UMEONEWA?
1. Baada ya kufanya kazi siku 30, unafukuzwa
kazi bila mshahara.
2. Ukiwa una download kitu kwenye net, inafika
99% alafu inagoma.
3. Unaingia na kibomu kwenye pepa alafu
unashindwa kuelewa mwandiko Wako
mwenyewe.
4. Unanunua simu Leo tsh elfu sabini alafu
kesho zinawekwa kwenye promo zinauzwa elfu
thelathini.
5. Unamualika Demu mkali kwenye dinner
unaagiza samaki alfu mwiba wa samaki
unakukaba kooni.
6. Unakamata manzi alafu unazama nae getoni
alafu unashindwa kusimamisha...
7. Unavunja uhusiano na boyfriend Wako alafu
siku inayofata ananunua gari aina ya vogue ya
shilingi milioni 90.
8. Unanunua pafyumu kali lakini kwapa bado
linatema.
9. Unafanya kazi kwenye kampuni miaka 10 bila
kupandishwa cheo na kuongezewa mshahara.
10. Unamdanganya mkaba roba kuwa huna
simu alafu inaita..
11. Unagombana na mtu barabarani alafu
kufika ofisini unapokwenda kuomba kazi
unamkuta anakufanyia interview.
12. Kama gari lako linatumia muda mwingi
gereji kuliko barabarani.
13. Kwenye pepa matokeo yanatoka umefeli
mathematics na kiswahili pia!!!....
14. Unaingia kwenye pepa alafu unasahau jina
lako la kwanza.
15. Unasajiliwa kama beki kwenye timu ya
barani ulaya alafu jaribio la kwanza unapewa
kumkaba Lionel Messi.
16. Kama mtoto Wako wa pekee anajiunga na
JWTZ.
17. Kama ukikosea ukaweka super glue
machoni badala ya dawa ya macho.
18. Kama utapiga picha photoshop
lakini bado unaonekana m'baya.
19. Kama panya atakula jina lako tu, kwenye
Cheti chako muhimu.
# Kati ya zote ipi ikitokea unakua umeonewa sana??
 
Samahan naongezea

20. Kununua king'amuzi cha star times kwa bei ya juu kwa ahadi ya kuweza kupata local channels bure kisha wanavipunguza bei local channels hupati customer care anakujibu huo mfumo wa free channels tumeuua.
 
Samahan naongezea

20. Kununua king'amuzi cha star times kwa bei ya juu kwa ahadi ya kuweza kupata local channels bure kisha wanavipunguza bei local channels hupati customer care anakujibu huo mfumo wa free channels tumeuua.
Huu ni uonezi mbaya zaidi
 
Unapoteza miaka 19 shuleni ili kua na maisha mazuri afu unakosa ajira!
 
Unapiga kura chama kingine halafu unambiwa CCM ndio wameshinda....
 
Hahaa. No.14.nliwahi kusahau kabisa neno 'capitalism' kwenye mtihani wa history..nikajikasirikia sikutaka kumuuliza mtu wala kuangalia notes mpaka siku mbili baadaye ndo nkalikumbuka
 
Namba 3: kuna mshikaji wng ndani ya NECTA F4, Geog. aliniuliza:

"Zanzibar ipo Africa Eeeeh?"

Mbaya zaidi akanifanya nianze kuisoma upya, pepa yote na pages zote, hamna sehemu yoyote ile ilipotajwa neno Zanzibar.

Nikatafuta labda ktk multiple choices, sikuona. Nikamjibu tu: NDIO.

Yule mshikaji wangu alinionea!
 
Kama mwenye nyumba anakuchaji sh 15000 ya umeme kwa mwezi humo chumbani kwako una TV tu ambayo inatumika usiku tu, inauma sana
 
# 6 - Inatokea hasa ukiwa na Malaria, ama kakuwekea tego.

# 16 - Naongezea, na yule aliyeenda upadre pia.

Vyote hivyo ni uonevu kwa kweli.

Ahsante!
 
21. Dah....unajenga mtandao ndani ya timu kwa miaka 20 halafu siku ya mechi unakatwa.....unahamia timu nyingine halafu golikipa na kiungo wanagoma kucheza nawe kisha timu inafungwa 🙂
 
Umedate na mwanaume miaka kadhaa anakupiga chini afu kabla hata hujajielewa anaoa baada ya miezi 6
 
Unaamua kupita shortcut njia ya chocho asubuhi ukiwa unaenda ofisini..kisha unakutana na dimbwi unazama,na engine inanoki.
 
Back
Top Bottom