Lazima uupende mlo huu

ameline

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
2,292
Reaction score
1,151
nilivutiwa na MziziMkavu na threa yake ya kuhusu pishi la bamia,.na kwangu ndo ilikua mara ya kwanza kujua kama inaitwa ladies finger, nshazoea okra mie kumbe !!!! basi katika pitapita yangu ya kuongeza maujuzi nikakutana na hii,. be careful with your tongue jamani, usijing'ate., KARIBU


[h=3]LEO NDIO NIMEJUA BAMIA KWA KIINGEREZA INAITWA ''LADIES FINGER''[/h]
Nilijua inaitwa okra lakini kumbe marekani ndio wanaita hivyo ila kwa kiingereza Ladies finger.
Kwa nini ziliitwa ladies finger?inasemekana ni kwasababu ya umbo lake lilivyo kama vidole vya mwanamke.
Bamia hukatwa na kupikwa kwa mapishi tofauti tofauti
Ukaipika kwa urefu kwa maana ya kukata kikonyo na ncha yakekisha kuiunga na nazi.​
Hizi zimewekwa tayari kwa kuokwa.Zimepasuliwa katikati halafu kwa ndani ukawekwa mchanganyiko wa vitunguu maji,jeera,coriender,pilipili ya unga,chumvi,mafuta ya kula,tangawizi na nazi vikachanganywa na kutiwa humo.Hii ni recipe ya kihindi ndio huwa wantengeneza hivi.
Huu sio mlenda bali zimekatwa ndogo ndogo zikaungwa vizuri kama zinavyoonekana...njaa inaanza kuniuma sasa maana ninavyopenda bamia.
Mlenda pale unahusika.....ukichanganya na majani ya maboga,nyanya chungu saafi unapika ladies finger zako.
India wanakula sana bamia....hii ni salad ambayo imetengenezwa baada ya kuziosha vizuri ladies finger zako.Unakata kikonyo unaziweka kwenye sufuria na maji kidogo halafu unazichemsha kwa dk 3 hvi ila zibaki kijani kama zilivyo.Unakatakata nyanya vidogo vidogo,vitunguu,pilipili,unatia chumvi,limao kama unavyotengeneza kachumbari.Baada ya hapo unakata bamia kama zinavyoonekana unatia hiyo salad yako tayari kuliwa.
Faida ya kula Ladies finger bamia
1.Inasemekana ni chakula kizuri kwa watu wenye msongo wa mawazo,wanaojisikia weak n.k
2.Ni chakula kizuri kwa wanaotaka kupunguza mwili.
3.Mbegu za bamia zina protine nyingi na mafuta
4.Inasaidia mmeng'enyo wa chakula na kupata choo vizuri
5.Zina vitamin A na C
6.Madini ya potassium,calcium na magnesium
7. Wataalamu wengine wanasema ni msaada kwa wenye matatizo ya vidonda vya tumbo kwani hupunguza acid mwilini


Kula bamia zako wala usizichukulie poa kisa zinateleza,ziko bomba kiafya.
 
eti Bamia ni dawa ya constipation, kweli MziziMkavu?

inaweza kusaidia kwenye constipation kwa sababu ni roughage.
Tatizo langu bamia zikikatwa katwa zinakuwa utelezi. Napenda bamia kupika nzima nzima na kuweka alongside viazi na nyanya chungu; kwenye nyama ama dagaa.
 
Last edited by a moderator:
deliciously., hata kama nilikua nimeshaaga nikiiona SIONDOKI HADI KIELEWEKE.
 
Hujeweka risep zake ndugu....nimependa hiyo ya pili inaoneka ni steamed
 
inaweza kusaidia kwenye constipation kwa sababu ni roughage.
Tatizo langu bamia zikikatwa katwa zinakuwa utelezi. Napenda bamia kupika nzima nzima na kuweka alongside viazi na nyanya chungu; kwenye nyama ama dagaa.
ni dawa ya wanawake
 
Nasikia kwa wanawake wale wenye tatizo la ukavu wakati wa tendo ni dawa inaleta utelezi huko ikulu bamia na nyanya chungu
ngoja nilete maelezo ya hiyo dozi hapa
 
ohh my....yani nimeshindwaje kujizuia mate yamejaaje mdomoni ohhh....
 
ni dawa ya wanawake

hasa wanawake wajawazito coz inarahisisha wakati wa kujifungua hujikakamui sana, utashangaa mara chap mtoto huyo, hii ni kwa mujib wa mama yangu jaman.hasa ujauzito wa miez 7 na kuendelea
 
Frankly speaking I dont like bamia
 
Nasikia kwa wanawake wale wenye tatizo la ukavu wakati wa tendo ni dawa inaleta utelezi huko ikulu bamia na nyanya chungu
ngoja nilete maelezo ya hiyo dozi hapa

hivi vibao kata vitakuchanganya shosti, ni myth tu hiyo! Ule utelezi ni function ya hormones aka vichocheo. Kubalance hormones kula chakula bora, fanya mazoezi na epuka obesity na kuugua kunakopelekea matumizi ya antibiotics, bhaaaas! Mengine ni urithi!
 
hasa wanawake wajawazito coz inarahisisha wakati wa kujifungua hujikakamui sana, utashangaa mara chap mtoto huyo, hii ni kwa mujib wa mama yangu jaman.hasa ujauzito wa miez 7 na kuendelea

hizo ni imaginations nadhani, sidhani kama kuna ushahidi wa kisayansi. Process ya uchungu kuanza na mtoto kutoka is a central dogma. Lakini kama bamia zitampa mama mjamzito courage ya kusubiria kujifungua, acha ale manake sio sumu.
 
Mie bwana bamia halipandi ng'ooooooooooo. Hata nikipika sionjiiiiii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…