Nikuumbushe kitu kimoja ndugu yangu, ni lazima maisha yako uwe kama chujio tena chujio la umakini kuchagua yupi wa kuwa nae karibu au kubaki nae katika safari yako ya mafanikio kwasababu hakuna anayeweza kukupiga kofi akiwa mbali na wewe na wala hakuna mtu anayeweza kukuambukiza mafua akiwa mbali na wewe.
Yule ambaye unaamua kuwa nae karibu ndiye ambaye anaweza kupiga kelele za kukupa moyo au kukukatisha tamaa katika mwelekeo wowote ambao atakuwa anaona unao katika maisha yako.