Masiya
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 7,602
- 7,332
Leo Jumatatu, March 19, 2018 atakuwa at Dancing bar 1,2,3 at Mama Kulutu, Alhamisi, March 22, ni Kamina street No. 24, Yolo North. Ijumaa March 23, Lutumba Simaro atapiga show yake ya mwisho ShowBuzz Hall iliyoko Colonel Mondjiba Avenue, Ngaliema Commune.
Simaro ni mpiga rythm mashuhuri wa OK Jazz na Bana OK, kwa wajuvi wa mambo huyu pia alikuwa mwalimu ndani ya OK Jazz kuanzia vijana wakina Youlou (1966) hadi wakina Malage de Lugendo (1980's). Lakini sifa yake kubwa ni katika utunzi-mfano ni Maya (iliyoimbwa na Carlyto Lassa), Mabele (iliyoimbwa na Sam mangwana), Dati Petroli (aliyoimba Madilu), Mbongo, Mandola, Kadima (alizoimba Djo Mpoyi) na utitiri wa record ambazo Josky Kiambukuta aliongoza waimbaji wa OK Jazz.Katika anga za utunzi yuko kule kwenye kundi la Franco na Tabu Ley. Lakini pia yeye ana mashairi mazito hadi kupewa jina la Le Poet.
Ame mentor wanamuziki wengi sana pamoja na Sarah Solo wa Werrason na Olivier Tshimanga mkali wa solo asiye na mfano-hawa wamepitia Bana OK. Ndani ya OK Jazz amekuwa mpiga rythm, Chef d'Orchestre, Vice President na mwisho kabisa President wa OK Jazz hadi bendi ilipovunjika. Kijana wa Luambo ameifufua miaka ya karibuni.
Nimtakie maisha mema nnje ya muziki baada ya kuwa kwenye game kwa miaka 60 wiki hadi wiki bila kupunzika labda alipokuwa na udhuru. Nyimbo zake na mashairi yake yataishi milele.
Update
Serikali ya DRC leo 19.03.2018 imemuenzi Simaro Lutumba kwa kubadilisha jina la Avenue Mushi kuwa Simaro Lutumba Avenue.
UPDATE
Papa Simaro Lutumba Ndoamanenu Masiya amefariki mjini Paris siku ya Jumamosi tarehe 30 March 2019 siku kama 11 baada ya kutimiza miaka 81. Mola aiweke pema Roho yake (RIP). Pole kwa familia yake, familia yake kubwa ya muziki na wapenzi wake.