Nashukuru kwa kupata hukumu hii. kama ndio nakala halisi ya mahakama, kama mwanasheria nimesoma critically facts na issues za judge alizotumia kufikia uamuzi wake. Kisha nimegundua mapungufu yafuatayo-
1. Judge anakiri Kamanda G. Lema hakutamka maneno hayo BINAFSI bali wawakilishi wake, hivyo nilitarajia judge angekuwa na additional issue ya kumtambua nani aliyetamka maneno hayo kwa niaba ya G. Lema; hakuna popote nilipoona anatajwa mtu huyo;
2.Jambo la pili ambalo judge hakulitatua ni kuhusu huyo mtu aliyetamka maneno ya kashfa dhidi ya mgombea wa CCM je alitamka maneno haya kwa kibali na ruhusa ya Kamanda G. Lema,je Lema alijua hayo yamesemwa na akayakubali kwamba hata ingekuwa yeye angefanya hivyo, maswali haya naona bado hayajajibiwa katika hukumu hiyo ya jaji, ndio maana alifikia uamuzi huo
3. Suala jingine ambalo jaji alitakiwa kulitolea tafsiri endapo kosa la jinai alilotenda A anaweza kuhukukumiwa B bila ya kushirikiki katika kosa hilo kufanyika,
4. Maneno mengi yaliyosemwa naona ni alleged defamation ambayo ina taratibu zake na fidia hutolewa pale inapodhibitika, itafaa CDM kuanza mchakato wa kuomba amendments ya kifungu hiki kwani kimejumuisha masuala mengine ambayo yanasimamiwa na sheria zingine na yana utaratibu wake wa fidia. hii itakuwa iliwekwa kwa makusudi na tayari huenda watu wa kutamka ovyo waliandaliwa bila upinzani kujua ili kupata sababu ya kutengua wabunge wa upinzani
Kwa mtizamo wangu haya masuala matatu yakitizamwa kwa upana wake kamanda G. Lema atarejea Bungeni hivi karibuni
CDM waongeze bidii ili kamanda arejee mjengoni kabla ya mjadala wa KATIBA MPYA
mm napita
Ili uweze kumshinda adui yako unapaswa kufahamu uwezo/fikra/mawazo na mbinu zake