Hii hukumu ni dhaifu sana kwa vile haikutokana na physical evidence yoyote, bali imetegemea testimony ya mtu mmoja tu. Kesi ilikuwa inatosha kabisa kutupiliwa mbali baada ya mashahidi kushindwa kuwa consistent, jambo linaloonyesha kuwa walifundishwa.
Huyo shahidi aliyeaminiwa inawezekana yeye kwa vile alikuwa afisa wa jeshi akawa anajua kutunza kumbukumbu aliyofundishwa, lakini hakuna sababu yoyote ya kuamaini moja kwa moja kuwa analosema ni la kweli kwani yeye si malaika; yupo pale mahakani kama sehemu ya walalamikaji.
Ilikuwa ni jambo la ajabu kuwa ushahidi ulioaminiwa na mahakama wa Omari Bokolo ulikuwa ni tofauti na ule wa mlalamikaji wa kwanza halafu mahakama ikaona kuwa yeye ndiye mkweli kuliko mlalamikaji. Ni kosa kwa mahakama kufikiria nje ya ushahidi na malalamiko yaliyoko mbele yake. Baada ya mashahdi kujichanganya kuhusu tukio moja, ilikuwa ni wazi kuwa ushahidi wao kuhusu tukio hilo haukuwa na thamani tena.
Kwa maoni yangu, naona kama Jaji aliianza na presumption ya kuwa Lema ni mkosaji, na hivyo kuweka burden kwa Lema kuprove otherwise, ila kama angefuata utaratibu halisi wa kisheria wa kuanza na presumption of innocence kwa Lema na kuwaachia walalamikaji burden ya kuprove beyond reasonable doubts, basi kesi hii ilitakiwa iwe imekwisha kabla ya mashahidi wa utetezi kupanda kizimbani.