Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Kutokana na harakati za uchaguzi na matokeo nafikiri sasa ni wakati wa kuendelea na maisha. Ni lazima tukubali kwamba Tanzania ni kubwa zaidi ya tofauti zetu za kisiasa na kwamba pale tunaposhindwana kwa kutumia mbinu A basi tukae chini tupange mbinu B na tuhakikishe kwamba Tanzania inaendelea kusonga mbele bila kujali tofauti zetu. Wale ambao wanahisi maisha yao sio salama na wameamua kuondoka nchini wamefanya jambo zuri kwa ajili ya usalama wao ila kwa sisi ambao hata uwezo wa kuondoka hatuna basi tuendelee kushirikiana na watesi wetu huku tukiongeza umakini na kupunguza uoga ili tuweze kusonga mbele kama taifa. SASA TUENDELEE na Mjadala wa MSINGI
Learning Curve au kwa kiswahili sahihi Uelekeo/Mtiririko/Mkunjo wa kujifunza hujitokeza pale ambapo mtu anaponza kujifunza kufanya jambo fulani huku akiwa analifanya. Kwa mfano kama wewe ni mjasiriamali basi katika zile hatua za mwanzo za biashara yako utatumia muda na gharama nyingi sana katika kujifunza. Hizi gharama na muda zinaweza kupungua iwapo kasi yako ya kujifunza itakuwa kubwa.
Kwa mfano kama utajifunza kwamba unaweza ukatumia mtu mwingine kufanya vile vitu ambavyo kwako ni vigumu basi utafupisha muda wako wa kujifunza. Kwa nini ni muhimu kujifunza jinsi ya kumanage learning curve. Ni kwa sababu unaweza kutumia muda na nguvu nyingi kujifunza jambo ambalo haliongezi thamani kwa biashara yako. Ukiweza kufupisha utatambua mapema iwapo biashara yako inafaa/inalipa au hailipi.
Kama mjasiriamali unatakiwa ufahamu kuwa unapojifunza basi ufanisi wako unaongezeka mpaka unafikia kikomo(Marginal Productivity) Hivyo basi ni muhimu sana ukatafuta namna ya kuwahi kufika hapa kwenye huu ukomo wa ufanisi ili uweze kufahamu kwa kina iwapo biashara yako inafaa kuendelea nayo. Kuchelewa kufikia katika hatua hii kunaweza kusababisha hasara kubwa zaidi kuliko ungewahi kufika.
Tujadili basi hapa kuhusu umuhimu wa kufahamu kuhusu Learning Curve na namna ambavyo unaweza kupunguza muda unaotumia kujifunza.
NB: Utangulizi nilioweka sio sehemu ya mjadala huu.