Messenger RNA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 1,411
- 3,712
Hali katika eneo la mpakani kusini mwa Lebanon inazidi kuwa tete, huku Israel ikishambulia kwa mabomu mji wa Bint Jbeil kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita kusini mwa Lebanon.
Kulingana na vyombo vya habari vya Lebanon, watu watatu waliuawa katika shambulio la bomu lililopiga makazi ya raia - mwanachama wa Hezbollah na watu wawili wa familia yake.
Katika maelezo hayo, ndege za Israel zilivamia nyumba ya familia ya Bazzi muda mfupi kabla ya saa sita usiku katika kitongoji cha Doura katikati ya mji wa Bint Jbeil, na kuiharibu.
Vikosi vya uokoaji vilipata miili ya kijana Ali Bazzi, kaka yake Ibrahim Bazzi, na mkewe.
Mtu mwingine wa familia moja pia alijeruhiwa. Ibrahim anaishi Australia na alikuja Lebanon pamoja na mke wake hivi karibuni.
Ving'ora vilisikika katika eneo la Galilaya Magharibi kaskazini mwa Israeli.
Kituo cha Channel 12 kiliripoti kuwa makombora yalirushwa kutoka Lebanon kuelekea eneo la Galilaya.
Chanzo hicho hicho kilieleza kuwa makombora 18 yalirushwa kutoka Lebanon kuelekea eneo la Ras Naqoura, na mfumo wa Iron Dome wa kunasa makombora ulizuia nane kati ya makombora hayo, bila kusababisha hasara yoyote.
BBC swahili