left hand drive motor vehicle.

left hand drive motor vehicle.

goldie ink

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
5,634
Reaction score
9,149
Habari wanachama wote wa jamii forums na viongozi wote kwa ujumla.

Naamini jamii forums ni mtandao bora wa kitanzania katika kujua habari mbalimbali katika jamii na kukufanya kuwa mmoja wapo wa ( The great thinker )

Moja kwa moja kwenye mada husika ni kuhusu matumizi ya magari ambayo usukani wake upo upande wa kushoto, lakini katika mfumo wetu wa miundombinu ya barabara ya Tanzania, na afrika ya mashariki kwa ujumla magari yana usukani ambao upo upande wa kulia, na vigumu ( left handed car ) kutumika katika barabara zetu japo chache zipo zinatumika nchini.

Mimi ni mhanga mmoja wapo ambao napenda kutumia magari yenye left hand drive, kutokana na mimi binafsi kutumia zaidi mkono wa kushoto hivyo mapenzi yangu ni kutumia gari za aina hii kwa miaka ya mbeleni.

Vile vile magari mengi ambayo watanzania na watu wa kanda ya afrika ya mashariki kwa ujumla kutumia magari ya right hand na kuagiza uingereza, Japan n.k kwangu gari ya mjapan bado sihitaji kutumia napenda nitumie gari ya mzungu ambazo mara nyingi hutoka ulaya na mfumo wake uwe kushoto, ( left hand drive )

Kwa ushauri zaidi ni maradha gani nitapata endapo nitatumia gari hizi za left handed car.

Vile vile itakuwa ni gharama kuagiza magari yenye mfumo huu wa left hand drive.

Asanteni wana greti thinkaz.
[emoji4] [emoji111]
 
Ngoja waje wajuzi zaidi, ila kwa kuchangia kidogo, sidhani kama kuna madhara makubwa kama unavyohofia ila ni ishu ya umakini tu kwa sana unapokuwa barabarani hicho ndo cha kuzingatia.
 
Nadhani wangezuia kabisa uagizwaji wa left hand drive magari, keep left....

Nchi nyingi waliamua hivyo, ukizingatia vibarabara vyetu vilivyo vyembamba.....
 
Nunua mzee.

Kwanza kuazimwa hakuta kuwepo.
 
Ukienda mkoa ukikuta roli lipo slow njian afu una left hand drive utakaa hapo masaaa hujaovateki mana upande wa kupitia huoni...
So sio busara kuwa na lefthand drive
Hahaha Hahaha umenichekesha mkuu, kwanza left handed car hutakiwi kumkaribia aliyeko mbele ili uone mbali kwa urahisi lakini pia unaweza kuitoa nje ya njia kidogo na baada ya kuhakikisha usalama ndiyo unaovertake..kwa ujumla gari hizi zinahitaji umakini zaidi
 
1. Kutumia mkono wa kushoto hakukufanyi kuendesha vyema gari la LHD, mimi ni right hand but naendeshea kushoto zaidi, fahamu sterling sio kalamu ya kuandikia.
2. Kutumia gari la LHD inahitaji umakini mkubwa sana kwenye overtaking, kona kali, kurudi nyuma... why wasting all your energy kwa hela yako?
3. Ukinunua LHD ndio umefunga nalo ndoa ikitoka kwako ni kuuza screpa....
4. Acha ulimbukeni wa ulaya.... hapa upo bongo.
 
Ukienda mkoa ukikuta roli lipo slow njian afu una left hand drive utakaa hapo masaaa hujaovateki mana upande wa kupitia huoni...
So sio busara kuwa na lefthand drive
hapo kuna shida sana hasa kwa wale wasio wazoefu!
 
Changamoto pekee nnayoiona ni kwenye entrances zinazofunguliwa kwa kadi au code ambapo zinakuwa upande wa dereva(kulia).

Mfano pale mlimani city Dar au entrance airports and some parkings.Mkiwa wawili hamna shida.

Ila mkuu hata kama unatumia mkono wa kushoto, hautapata shida kuendesha RHD.LHD au RHD ni utaratibu tuu na hauangalii kwamba driver anatumia mkono gani....
 
Back
Top Bottom