Legacy: Waimba Mapambio Wanapokwama

Legacy: Waimba Mapambio Wanapokwama

Chawa kama hawa ni Very Very Dangerous
notagain1.png
 
21 May 2020 — "Niwakumbushe mabalozi kuwa balozi namba moja ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ... Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania anasema ..source : twitter.com

Professor ametupiwa lawama, ingawa ni balozi namba ngapi vile? Maana kila nchi ina balozi namba "moja" katika ulimwengu huo wa kuwakilisha mahusiano na muonekano wa nchi yake .

Toka maktaba :
10 January 2020
Balozi namba "mbili" aelezea changamoto za kidiplomasia na jinsi ya kwenda nazo ili ziwe fursa


KAULI ya Waziri KABUDI, BALOZI wa KENYA Kuhusu USHIRIKIANO na MATAIFA Mengine Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, amezungumza na wanahabari kuhusiana na ushirikiano wa Tanzania na nchi za Afrika mashariki.
Source : Global TV online
 
Kila tawala ina kipaumbele chake kutokana na nyakati zilizopo, changamoto, fursa, michezo ya kisiasa nk
 
Chawa kama hawa ni Very Very Dangerous
View attachment 2001874
Sema tena na tena na tena. Na wako wengi kweli kweli. Hawa ndiyo ma-DC watarajiwa. Kweli inabidi turudi kwenye maombi sasa ila Mungu aingilie kati kutunasua kutoka kwenye hili tope tuliloingia. Yaani kwenye siasa na uongozi kumekuwa ndiyo makao makuu ya wajinga na weruvu na wenye akili wamebaki mitaani kusaga lami! Hivi mna uhakika huyu siyo yule naibu supika wa bunge jamani?
 
kwani mama haupigi mwingi tena ndugu zangu nyumbu??!
 
Kijana mwenzangu ameelezea vyema tu.....

Komredi wetu ametambaa kiuhalisia kabisa........

Awamu ya 6 ina kiongozi ambaye anajua vyema thamani ya DIPLOMASIA na MAWANDA YAKE iliyomsukuma kututeulia WAZIRI BOBEZI WA MAMBO YA NJE mh.mama Liberata Mulamula......

Ndani ya MUDA mfupi tu BOBEZI LA DIPLOMASIA mh.Mulamula ametuletea huyu hapa......huyu......


#Siempre JMT
E65OMZ3WEAkIWlV.jpg
 
Haka kajamaa kanaonekana kana uwezo wa kumkana hata mama yake mzazi kama kuna maslahi binafsi.
Unamsingizia....

Huyo ni MWANASIASA....anaongelea uhalisia wa mambo yalivyo.....

Kwani aliyoyasema ni uongo?!!! 😳🤣🤣

Siempre JMT
 
Mbatia ameshasema kuwa nchi inapitia kigumu mana inakabiliwa na janga la uongozi. Huyu soon atateuliwa kuwa DED au DC hajui hata anavhokiongea.
 
Mbatia ameshasema kuwa nchi inapitia kigumu mana inakabiliwa na janga la uongozi. Huyu soon atateuliwa kuwa DED au DC hajui hata anavhokiongea.
Kwani maongezi mema ni lazima yawe yale yenye kufurahisha mtazamo wako?!!!
 
"Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko" - mwanaCCM / TANU

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) NEC, Jaffari Kubecha ameamua kutumia ahadi ya mojawapo ya mwanachama wa CCM kuwa - "Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko" mwisho wa nukuu.
Chama cha TANU ni chama kilichosaidia sana katika harakati za kuikomboa nchi yetu katika makucha ya ukoloni chini ya Uongozi madhubuti wa Hayati Julius K. Nyerere.

Malengo makubwa ya chama hiki ilikuwa ni ukombozi wa nchi yetu lengo ambalo kwa kiasi kikubwa lilitimia.Kinachonofurahisha sana ni jinsi viongozi wa TANU walivyokuwa na dhamira za kweli na kujitolea kwa hali na mali katika kuikomboa nchi yetu.

Lengo kubwa la post hii, ni kuwakumbusha wana JF Ahadi za Mwana TANU, na kama bado ni relevant kwa wakati huu ambapo Tanganyika(Tanzania) imefikisha miaka 49 ya uhuru, zifuatazo ni ahadi za Mwana TANU enzi hizo:




F25663D5-A6EC-4E4C-B4C1-122C4D9214A6.jpeg


1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.

5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.

8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika na Afrika.

10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika.
Source : Ahadi kumi (10) za mwana TANU na Tanzania yetu ya sasa
 
Back
Top Bottom