"Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko" - mwanaCCM / TANU
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) NEC, Jaffari Kubecha ameamua kutumia ahadi ya mojawapo ya mwanachama wa CCM kuwa - "Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko" mwisho wa nukuu.
Chama cha TANU ni chama kilichosaidia sana katika harakati za kuikomboa nchi yetu katika makucha ya ukoloni chini ya Uongozi madhubuti wa Hayati Julius K. Nyerere.
Malengo makubwa ya chama hiki ilikuwa ni ukombozi wa nchi yetu lengo ambalo kwa kiasi kikubwa lilitimia.Kinachonofurahisha sana ni jinsi viongozi wa TANU walivyokuwa na dhamira za kweli na kujitolea kwa hali na mali katika kuikomboa nchi yetu.
Lengo kubwa la post hii, ni kuwakumbusha wana JF Ahadi za Mwana TANU, na kama bado ni relevant kwa wakati huu ambapo Tanganyika(Tanzania) imefikisha miaka 49 ya uhuru, zifuatazo ni ahadi za Mwana TANU enzi hizo:
1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.
2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote
3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.
4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.
5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.
7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.
8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika na Afrika.
10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika.
Source :
Ahadi kumi (10) za mwana TANU na Tanzania yetu ya sasa