Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

 
Hekima zake, busara zake, uchamungu na uungwana wake unamfanya kuwa best president ever so far in this country
 
Halafu kuna njemba ilimkataga mabanzi mubashara hadharani yaani watu wana laana dunia hii.

Na upole ule wa Mzee mwinyi unatoa wapi ujasiri wa kumuadhibu na sucker slap...alinifurahisha alipomsamehe. That's was tottaly humane and humble.
Hivi hili neno "mubashara" lina maana gani?
 
Mkuu kinacho nishangaza ni kuwa mfumo wa vyama vingi sifa nyingi anapewa Nyerere wakati aliyekuwepo madarakani ni Mwinyi sijajua kwa nini anasifiwa Nyerere
Duh , ndugu mbona hiyo haipo. NYERERE ndiye aliyeleta siasa ya chama kimoja. Na uzuri wake alikuwa hapendi upinzani , ukimpinga basi unapotea ksiasa na hata kimali.

He was not a cruel dikteta, bali alikuwa dikteta asiyesahau na kusamehe. Kuna waziri aliyetokea upareni ( nadhani alikuwa MGONJA ), alishindwa kufanya kazi na nyerere akaamua kufanya biashara, alifungua Butcher kwao (SAME), basi nyerere aliwa Finance watu kushindana nae kwa kuuza nyama kwa bei ya hasara mpaka mgonja alifunga kazi.

Nyerere alikuwa anakumaliza taratibu na tena huku anacheka.
 
Dah kumbe Mzee Mwinyi kafanya mengi hivi ya maana halafu hatujuzani watu wamesubiri hadi atutoke ndio waanze kumsifia na kumpamba! [emoji15]

Hongera Mzee Mwinyi Mungu akubariki sana aisee [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Nyerere alipoacha Urais alibaki mwenyekiti kwa miaka miwili hadi 1987
mwenyekiti wa CCM....

Umekosea kidogo hapo kwenye timeline.

Nyerere aliongoza C.C.M. muhula wote wa kwanza wa utawala wa Mwinyi, mpaka mwaka 1990 ndio akang'atuka.

Wanahistoria wengi wa Marais wanakubaliana kwamba Mwinyi alihitaji a steadying hand kutoka kwa Mwalimu ndio maana hakukuwa na shinikizo kwa Mwalimu kuachia hatamu za chama kama ambavyo Kikwete alishinikizwa kumuachia Magufuli chama ndani ya mwaka mmoja. Peke yake kabisa toka 1985 Mwinyi angeweza kuyumba.
 
Sikua najitambua ila waliontangua home haswa kakaangu mkubwa hua anatuhadithia naman mzee huyu alivyosaidia Taifa na wanyonge,maana inasemekana kabla yake hata wali tu kula ilikua anasa kubwa yaani mpala sikukuu za Idd na Crixmas,mahitaji ya muhim kama sabuni,sukar yaliuza ktk duka la ushirika na ilikua kwa foleni watu walivaa magunia maana ilikua ukikutwa na shati la mtumba moja ama mawili lazma jela ikuhusu,mzee katufungua sana macho kwa uongozi wake japo kizazi cha kulalamika huwa kipo tu,matajiri wa nchi hii wanaoonekana wengi wameibuka enzi za huyu mzee na ndio hapo ambapo wale wazee wa sasa ambao ndio walikua vijana kipindi hicho waliochangamkia fursa sasahivi wanakula bata huko masaki na kwingine,ila kwa wazee ambao walilala na wengine kua busy na madem sasa wamegandwa na umasikini
 
kwani umeshindwa kuuliza mazuri yake pasi kusema kabla hajafa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…