Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Mkuu nakuunga mkono kabisa sample yangu kuna mjuu wake binti mdogo tu anaitwa Sitti Mwinyi naweza kukapa nidhamu A.
Heshima kwa wakubwa iko vizuri sana hakuna nyodo kabisa, heshima to the family kwa kweli.


hili inaonekana ni kweli kwa sababu lina ushahidi wa watu zaidi ya watatu sasa kwa namna tofauti, Mungu ampe siku nyingi yeye na familia yake...
 
Mzee Mwinyi alikataa kuitwa mtukufu rais maana mtukufu ni Mwenyezi Mungu pekee na badala yake litumike neno ndugu (Rais wa Tanzania ndugu Ally Hassan Mwinyi)
Pia alisema nitakula mcicha na wananchi wangu! kwamaana na kupata shida na raha pamoja na wananchi wake.

Mungu amjaalie maisha marefu hapa duniani na kesho ampe maisha mazuri akhera! aamina
 
pale alipoita timu ya taifa kichwa cha mwenda wazimu,, mpka sasa timu yetu imeshindwa kufurukuta.. nimuombe tu atengue hyo kauli tupate kufanya vizuri kama zamani

Siku ikipata ushindi mnono waende wakaraguliwe (Kiluguru).

Kuna yule jamaa kule Marekani alikatazwa assingie na mbuzi wake kushanglia timu yake akaishia kuilaani..... Tim hiyo imehinda juzi baada ya miaka hamsini. Duu mdom* huumb*

Story haifanani haifananini lakini.
 
Mwinyi hakuwa na kibri alipokuwa Raisi na wala hakutaka ionekane Uraisi kama umungu vile, aliwakaribisha watu ikulu na kuongea nae, na hata baadhi ya watu walipata bahati ya kumuomba msaada kwa kumfuata ikulu, alijua yeye ni binadamu kama bnadamu wengine hivyo na majigambo kwake hayakuwa na nafasi, alikuwa mvumilivu sana, kuna kipindi cha uraisi wake kuna baadhi ya wanafunzi chuo kikuu walidiriki kumchora mchoro ulioonyesha anajisaidia haja kubwa. Mwinyi kwa upole wake baada ya kuwafukuza chuo lakini muda si mrefu akawarudisha huku akisema na msemo wake..“mtoto wako akikunyea mkononi, huwezi kuukata mkono bali utaosha''.
Wakati anaaga kipindi cha kumalizia uraisi wake pale uwanja wa taifa mwaka 1995 alisema .“anaondoka kiongozi atakuja mtawala,'' na alisema maneno kuwaambia wale wote wanaompakazia ya kuwa kila kitu juu yake na mkewe bibi siti. Aliwaambia .''kila nyumba kubwa nzuri ni ya bi Sitti na huku akisema kuwa mkewe amevumilia mengi''
Na mwisho kabisa aliwaambia ''mutanikumbuka''
Kwa ufupi tuu huyu mzee ni wa kuigwa sana. Uchamungu wake umemfanya yeye ajione si lolote si chochote mbele ya viumbe kwa vile anajua fika hawezi kuwa yeye ndio bora kulilo wengine mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya cheo. Wapo waliokufa wenye kusifika na kila aina ya sifa sembuse yeye. Ule uoga wake juu ya aliyemuumba ndio uliondoa kibri na kijiweka chini mpaka ikafikia watu wengi wakimpenda ingawa wapo waliochukizwa nae na hapa watakuja kuleta dhana au kueneza propaganda au hata kulazimisha asionekane hakufanya kitu kwa sababu wanazojua wao wenyewe.
 
Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
IMF ndio waliozuia watanzania wasiende ulaya kuatafuta bidhaa ? WB ndio waliowalazimisha watu wasiwe na tv awe nayo mtu mmoka nchi nzima ? Hata sabuni zakuogea zilikiwa shida watu walifulia majani ya mpapai hili nalo nililkuwa ni katazo la IMF watanzania wafulie mipapai ?

Zile njozi za mchonga angezileta kipindi hiki angeungana na lema gerezani
 
...Si bora ukae kwenye foleni, baadae upate hiyo ration yako/yenu. Unaweza kaa, foleni ndio imetoa wanne, mnaambiwa "unga wa ngano umeisha". Dah, chapati ilikuwa anasa!

...Acha sukari au mchele. Unakumbuka sabuni nayo ilikuwa shida?
Nakumbuka Mchungaji Mtikila alilia kuuzwa kwa Tausi wa ikulu na kuuzwa kwa Loliondo kwa mwana wa mfalme
 
Katika hiyo picha, kwa nini jeikei amekaa katikati
 
Uzi huu wale wasiompenda mwinyi kwa ajili ya dini yake wana mengi ya kusema huku wakifumbia macho maovu ya nyerere na kumimina sifa nyingi na utakatifu juu, wakati ukweli upo wazi, Nyerere alitufanya tutembelee viatu vya matairi ya gari, tule dona la njano tena upatikanaji wake mbinde, watu walikuwa wakivaa kaniki kama waganga wakienyeji vile.
Hakuna aliyethubutu kusema lolote alikuwa dikteta anayepewa sifa ya utakatifu.
 
Ndiye Rais pekee mstaafu ambaye alikuwa Taifa kumsupport Magufuli. Wale wengine walijifanya bize nje ya nchi
 
Hii namba nne umekurupuka , hili sakati lilitokea mwaka 1998, je mwinyi alikuwapo? aliyeamrisha alikuwa sumaye je mwinyi alikuwapo, acha chuki zisizo na mpango,
 
Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!

Mzee Mwinyi, ni baba mzuri kwa watoto wake, mme bora kwa mke wake, babu mpole na msaidizi kwa wajukuu zake, nadhani alikuwa mwalimu makini kwa wanafunzi wake, jirani mwema kwa waliomzunguka, binadamu mstaarabu wa hali juu na binadamu wenye bahati nzuri sana kuliko binadamu wengi lakini hakuwa rais bora. Chama alichokiongoza kilipora ushindi wa Mhe. Augustine Lyatonga Mrema. Na kuanzia hapo domekrasia imehujumiwa kwa kiwango ambacho itachukua muda kuirejesha demokrasia iliyo kusudiwa.
 
Hatuongelei legacy ya Nyerere, weka uzi wa Nyerere uone kama hawatamchana!
 

Nnazitafuta sana hizo hotuba za Mwinyi na wazee wa Dar, hususan zile mbili za mwanzo.

Ukizipata nijulishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…