Leicester City, Special Thread

Husomeki kabisaaa!!!
Hahahaha dah mtu wangu wa nguvu, kwanza nimekumiss mno, halafu sio kama sikuoni kule jukwaa pendwa la MAN U nakuona sema nashindwa kupiga vigelegele furaha vijana wameiminya maana matarajio yamezidi uhalisia, humu kwenyewe moja haikai mbili hailali.. [emoji13]
 
Natamani hiyo nafasi ya Leicester tupewe Man U
 
Ujagee hata kunifariji best yangu.....
 
hongereni kwa ushindi wa jmosi na poleni kwa kichapo cha jana...
 
Ndugu zetu kwema humu mbona kumepoza?
 
Leo tumekunywa damu ya Fox , kumbe ina sukari nyingi aisee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndugu zetu kwema humu mbona kumepoza?
Wenyewe wapo busy, wanajitayarisha kushuka daraja.

Kuna kaharufu ka kushuka daraja na kwenda kwenye championship msimu ujao.
 
Wenyewe wapo busy, wanajitayarisha kushuka daraja.

Kuna kaharufu ka kushuka daraja na kwenda kwenye championship msimu ujao.
Wajitahidi wakaze game zao zilizobaki, me wananishangaza kwenye UEFA wamejitahidi ila kwenye Premier huko ndo wanahemea mashine, ila bado wananafasi wakaze buti tuuh.
 
Ranieri alishasema hili lililotokea msimu wa 2015/ 16 hujirudia kila baada ya miaka 20-28. Msimu huu wa 2016/ 17 ni wasindikizaji tu. Wenye karamu ni West Ham, Tottenham, Timu ya Malafyale (majogoo ya msituni), Arsenal na Chelsea.
mtani bahati Mbaya mimi nimechanjia Red kabisaaa!!!msimu ujao tunawapokea kombe
Leicester City ijitayarishe ku-beat Chelsea's record of finishing at 10th spot after winning the league in the previous season. Bye bye Leicester City.
Link Leicester City, Special Thread
Wameshahamia timu za man city na man united. Lakini sitegemei timu hizo zitabeba ubingwa wa msimu huu.
Leceister wajitahidi wasishuke daraja...wameishiwa pumzi kabisa
 
Kutoka ubingwa wa EPL msimu uliopita mpaka kupigania kutoshuka daraja msimu huu, haya mambo nilizoea kuyaona ligi ya Ujerumani timu inabeba kombe halafu msimu unaokuja inashuka daraja au inapigania kutoshuka daraja.

Ukiangalia Leicester City ya msimu huu iko hoi taabani huwez amini ni timu iliyobeba kombe msimu uliopita kila mtu anajipigia tu na ukiangalia hawajauza wachezaji sana zaidi Ya N'golo Kante.

Kwa hali ilivyo yaonesha rasmi N'golo Kante ndio alikua KIFARU pale City kwan tangu aondoke safu ya kiungo imepwaya kabsa hata kama ni uchovu wa wachezaji sio kihivyoo.

Je, kosa la Leicester City ni kumuuza N'golo Kante au mbinu za kocha zimefika kikomo?
 
wataalamu wa mpira walisema hili jambo la Leicester City kuchukuwa ubingwa ni la mara moja kwa miaka 100,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…