Leicester City, Special Thread

Hadi kufikia hatua hii ya EPL, composition ya fans wa Leicester City wa hapa Tanzania ni kama ifuatavyo:

1. Supporters wa Chelsea wapo zaidi ya 95%
2. Supporters kutoka timu nyingine hawazidi 5%
3. Supporters asilia wa Leicester ni 0%

Tunakoelekea inawezekana hizo % za Chelsea zikahamia ManU!!
 
Yeah! Kwa BPL, bado pabichi sana muda huu. Ikifika huko Feb, hata akina Aston Villa (Timu za mkiani) huwa wanaamka na kuifanya ligi kuwa tamu.
Aston Villa wanaanza kutoa dozi kuanzia mechi inayofuata.

Na Leicester anapata sare.
 
ok mkongwe wa football and especially england. umeshindaaaaaa
 
Anachukua kama tukuyu walivyopanda na kubeba ndoo
 
Anachukua kama tukuyu walivyopanda na kubeba ndoo
kuna watu washakariri kama ilivyo constant ya pie 3.14 au formula ambazo hazitobadilika kamwe kwamba. Arsenal,chelsea,man u na city na liver ndo wenye haki miliki. Ni ngumu sana kwa bundesliga,la liga,league 1 na serie A.kwamba timu iliyokaribia kushuka daraja msimu uliopita. eti iongoze kwa mzunguko wa kwanza mzima afu bado mbaki mkiamini mitimu mikubwa? wapenzi wa premier kazi wanayo
 
duh, haya sasa ni maajabu katika ulimwengu wa kandanda!!
 

Kwenye huu uzi sijaona anayebisha na kukataa kuwa Leicester hawawezi chukua ndoo, WANAWEZA KUCHUKUA NA NDIO UTAMU WA EPL. Ishu hapa ni eti leo watu wa hapa Tz wanadai ni die hard Leicester fans!
 

EPL kwa sasa ni ngumu sana kwakua kwenye kipato gap ya mkubwa na mdogo ni ndogo sana. Kama mkubwa anaweza nunua wa 40 mdogo anaweza kununua wa 10. Timu zipo average sasa ukizubaa unapigwa tu maana hakuna namna.
 
EMT yupo wapi jamani? Kitambo kweli sijamuona. Angeweza kuijazia nyama hii thread.
 
Last edited by a moderator:
mi ningeshauri huu Uzi utumike kwa ajili ya timu ndogo ndogo ambazo hazina thread humu au EPL in general, pia kwajili ya Transfer rumors kuelekea dirisha dogo la usajili hapo January.

mtazamo tu
 
Mimi nilianza kuifuatilia Leicester season ya 96-97 walikuwa wana mturuki mmoja anaitwa muzzy izzett alikuwa balaa sana yaani kama unavyomuona paollo di canio mtata na mtupiaji Mzuri.long live the foxes
 
Hii timu ikichukua ubingwa natembea uchina yaani utupu tazara mpaka ubungo, Mwaka jana soton iliishiwa pumzi second round, ngoja tuone hawa Leicester city
 
Naona kuna wanazi wa hii timu ambao najua bila shaka wamechoshwa na maumivu ya hukooo kwenye 'timu zao' za ukweli. Sio mbaya kwani mwanadamu ana asili ya kutafuta furaha popote pale inapopatikana. basi ngoja niiongezee nyama hii profile ya timu tishio kabisa kwa sasa katika EPL.


Leicester City Football Club
Nickname: The Foxes
Founded 1884; 131 years ago
(as Leicester Fosse )
Ground King Power Stadium
Capacity 32,262
Owner King Power international
Chairman Vichai Srivaddhanaprabh
Manager Claudio Ranieri
League Premier League
 
Mimi nilianza kuifuatilia Leicester season ya 96-97 walikuwa wana mturuki mmoja anaitwa muzzy izzett alikuwa balaa sana yaani kama unavyomuona paollo di canio mtata na mtupiaji Mzuri.long live the foxes

Alikuwepo pia Rob Savege msumbufu na mkorofi pia, akizifunga nywele zake kwa nyuma. Kwa sasa ni mchambuzi wa soccer pale BBC.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…