Heshima kwako PakaJimmy,
kwanza naomba kukushukuru kwa jinsi unavyochangia hoja unamfanya mtoa hoja kusoma mara mbili kabla ya kujibu natumaini wengine watajisahihisha na kufuata mwelekeo wako.Kabla sijaanza kukujibu naomba usisahau,usidharau,usishawishike tarehe 31/10/2010 kapige kura wewe,mkeo,beki tatu,jirani na marafiki Dr W Slaa anahitaji kura yako ushabiki pekee bila kura ni kazi bure.
Mkuu nilianza kumpinga Lema siku nyingi hata kabla hajajiunga CHADEMA,alipojiunga nilitoa angalizo kwa chama wawe makini na sababu nikazitaja bila kuongopa,mambo mengi niliyosema yamedhihirika na mbele ya safari mtasikia mengi.
Mkuu hivi Lema kushikiliwa na polisi kwa kujipatia fedha isivyo halali ni habari zisizotakiwa jamvini ?.Tunatakiwa kuleta habari za kumsifia tu ?.PakaJimmy naamini JF haiko hivyo ila kuna watu wanataka kutulazimisha tuwe hivyo nina hakika mimi,wewe na great thinker wa kweli hawatakubali.Tunategemea CHADEMA kishike madaraka hivi Lema akipewa uwaziri atakuwa na tofauti gani na akina Karamagi ? mtu anyetapeli watu akikabidhiwa dhamana usitarajie ataacha utapeli badala yake tutarajie atakuwa tapeli mkubwa zaidi kwasababu atakuwa na uwanja mzuri na mkubwa wa kufanya utapeli.
Mkuu unajua Mama Maimuna Rashid ameathirika kiasi gani kwa kutapeliwa na mtu tunayempigania aende mjengoni,unaweza kukuta kashindwa kumpeleka mtoto chuoni hilo hatulioni wala hatutaki kusikia mtu akisema na anayelisema atapewa majina yote mabaya unayoyafahamu na usiyoyafahamu.
Mkuu chama kinachotarajiwa kuleta mabadiliko lazima kihakikishe kinakuwa na viongozi sahihi[wasafi] ili waweze kusimamia mabadiliko hayo vyema.chama ni watu bila watu hakuna chama, watu wasafi,waadilifu,wabunifu na elimu nzuri ufanya chama kiwe kizuri.Mwl Nyerere aliwahi kusema "Utajiri unaotokana na wizi wa mali ya umma,na wizi wa fedha za kigeni na unyonyaji na uharamia wa aina mbalimbali hautupunguziii umaskini wetu,bali unaongeza.Chama chetu hakiwezi kukubali hali hii na kikaendelea kuwa CCM,na wala kisitazamie kuwa wananchi watakikubali" .Mkuu Pakajimmy CCM imejaa viongozi wabadhirifu wa mali ya umma,wezi,waongo,wasiojali maslahi ya taifa ndiyo maana tulimsikia Chenge akijibu kwa dharau mamilioni aliyoweka kweny account za nje ni vijisenti,tulimsikia Mramba akiwatukana watanzania kwamba ndege ya rais itanunuliwa hata ikibidi tule majani,tulimsikia Lowasa akillalama kaonewa pamoja na kuliingiza taifa hasara kubwa kupitia mradi wake wa Richmond.Hawa ni watu wanaounda ule mkusanyiko wa chama kinachoitwa CCM.CCM kimekuwa chama kibovu kwasababu ya kukumbatia watu wa aina hii,hawakutaka kutenda maonyo ya Mwl Nyerere kimefika mahali ambapo hakikubaliki tena sana sana wanalazimisha kama Kibaki au Mugabe.Mkuu PakaJimmy pamoja na Lowasa,Karamagi,Mramba,Chenge na nk kufanya uharibifu mkubwa lakini bado wana watetezi wengi kuliko unaweza kufikiri.Mkuu PakaJimmy ikiwa CHADEMA wataendelea kulea matapeli tofauti yake na CCM itakuwa haipo matarajio makubwa ya wananchi juu ya hiki chama yatatoweka kama mvuke nasisitiza lazima CHADEMA kichague watu wasafi ili kibaki kuwa chama safi na imara.
Wapo wapiganaji wengi wazuri ambao nina hakika wakifanikiwa kuingia bungeni hatuataliona pengo la mpiganaji wetu Dr W Slaa mfano mzuri ni mgombea ubunge Arumeru mashariki jina limenitoka anampeleka mbio Mhe Sumary isivyo kawaida kama wizi wa kura ukidhibitiwa nina hakika tutamwona Zitto mwingine mjengoni.Pamoja na kashikashi anazopata Sumary sijasikia mpinzani wake akiandamwa kwa kashfa yoyote eti kwasababu anaelekea kushinda ! .