Pre GE2025 Lema: CCM kukataliwa mkutano wao Ngorongoro ni Maigizo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000

“Kwenye suala la Ngorongoro, ilitakiwa twende huko kesho Ijumaa kwenye Mkutano, tuliomba mikutano mitatu, Makalla (Mwenezi wa CCM Taifa) alivyoona akatoa ratiba ya mkutano, nikamwambia Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini kuwa Makalla ameitoa hiyo ratiba makusudi, hawa wana mpango wa kutunyima sisi, wanataka kuweka mizania sawa kwamba wamewanyima na CCM, Hakuna polisi wa wilaya mwenye uwezo wa kuzuia mkutano wa Mwenezi wa CCM, hayupo, ni maigizo yale.

Pia soma: Kwahiyo wamezuia mkutano wa CCM ili kuhalalisha zuio lao kwa CHADEMA. Mnaweza kufanya zaidi ya hivi, hii ni aibu

“CCM walisema wanakwenda Ngorongoro tarehe 04 Septemba, sasa CCM hiyo barua ya kuomba mkutano waliipeleka lini? Yaani barua ya tarehe 04 unaipelekaje wiki hii yaani barua ya tarehe hiyo unaipelekaje mapema hivyo? Kwani wewe ni UDP una wasiwasi kuwa utanyimwa, CCm wana mbinu zisizofaa, kimsingi ni kwamba Wamaasai wamedanganywa”- Lema ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari mkoani Arusha siku ya Alhamisi Agosti 29, 2024.
 
“Kwenye suala la Ngorongoro, ilitakiwa twende huko kesho Ijumaa kwenye Mkutano, tuliomba mikutano mitatu, Makalla (Mwenezi wa CCM Taifa) alivyoona akatoa ratiba ya mkutano, nikamwambia Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini kuwa Makalla ameitoa hiyo ratiba makusudi, hawa wana mpango wa kutunyima sisi, wanataka kuweka mizania sawa kwamba wamewanyima na CCM, Hakuna polisi wa wilaya mwenye uwezo wa kuzuia mkutano wa Mwenezi wa CCM, hayupo, ni maigizo yale.

“CCM walisema wanakwenda Ngorongoro tarehe 04 Septemba, sasa CCM hiyo barua ya kuomba mkutano waliipeleka lini? Yaani barua ya tarehe 04 unaipelekaje wiki hii yaani barua ya tarehe hiyo unaipelekaje mapema hivyo? Kwani wewe ni UDP una wasiwasi kuwa utanyimwa, CCm wana mbinu zisizofaa, kimsingi ni kwamba Wamaasai wamedanganywa”- Lema ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari mkoani Arusha siku ya Alhamisi Agosti 29, 2024.
Ccm ni wajinga sana
 
Back
Top Bottom