Lema: Mbowe bado ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama na yuko kwenye group la WhatsApp mijadala yote kuhusu kesi anaiona

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mwanasiasa na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Godbless Lema amefanya mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha leo Novemba 1, 2026, ambapo amefafanua kuwa Freeman Mbowe bado ni mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA kwa mujibu wa katiba ya chama hicho. Lema ameeleza kuwa Mbowe yuko kwenye kundi la WhatsApp la Kamati Kuu na anasoma mijadala yote inayohusu chama na kesi zinazoendelea.

Akijibu hoja mbalimbali, Lema amewapuuza wale wanaodai kuwa kuna siri zinazovuja kwa Mbowe, akisisitiza kuwa kiongozi huyo hana haja ya kutafuta siri za chama kwa njia za siri kwani katiba inampa haki ya kuwa mjumbe na kushiriki moja kwa moja katika vikao vya Kamati Kuu.

Your browser is not able to display this video.
 
Kwanini haendi mahakamani kuhudhuria kesi ya mwenyekiti wake?

Kwanini mikutano na makusanyiko ya serikali(CCM) anahudhuria tena mbali mno na anapoishi wakati mwenyekiti wake mahakama inayosikiliza kesi yake haiko umbali hata wa km 5 na hafiki kutoa ushirikiano?
 
Kwa sababu Lisu Hataki Strategic engagement Sasa ataenda Mahakamani kufanya nini?Ili Aonekani na watu?
 
Kwa sababu Lisu Hataki Strategic engagement Sasa ataenda Mahakamani kufanya nini?Ili Aonekani na watu?
Na ameikazania hiyo strategic engagement balaa.
Kwa kifupi nilivyomsikia, siasa za ccm zilikua sana sehemu ya chadema kabla ya Lissu kuwa mwenyekiti.
Yan zile habari za kuoiga simu mtu aachiwe Lema kathibitisha hata cem wamekua wakifanya hizo, ila nadhan tofauti ni baada ya Mwenyekiti kubadilika na hizo habari za shortcut kutopewa priority tena ,siasa za baadhi ya watu ndani ya cdm imekua shida
 
Sasa Watanzania Wanataka nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…