Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Makada na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameendelea kutoa maoni juu ya hali ya sasa ndani ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa uongozi hasa ule wa nafasi ya uenyekiti taifa.
Godbless Lema, mwanachama wa muda mrefu na kada wa CHADEMA, ameandika ujumbe wa kina kupitia ukurasa wake wa X, akitoa wito kwa wanachama kutafakari kwa makini mwenendo wa maadili ndani ya chama.
Pia, Soma: Godbless Lema: Mbowe ameniambia zaidi ya mara 5 amechoka anataka kuachia Chama hiki
Katika ujumbe wake, Lema amehoji tabia za uongozi na ushindani ndani ya chama hicho, akisisitiza kuwa chama kikuu cha upinzani kinapaswa kujitofautisha na tabia za kimaadili zinazokinzana na malengo ya mabadiliko.
"Tafakarini kwa makini tabia za chama chetu kwa sasa... Ushindani ndani ya chama unatukuza maadili na malengo yetu kama chama cha siasa kinachotaka mabadiliko? Je, sisi na CCM tofauti yetu ni nini?" ameandika Lema.
Ameeleza kuwa uimara wa chama unatokana na maadili na usafi wa viongozi na wanachama wake, huku akionya dhidi ya matumizi ya rushwa katika mchakato wa kuchagua viongozi.
"Uimara na ukubwa wa chama unajengwa na maadili na usafi wa viongozi na wanachama wake na wala sio mtandao wa matawi. Uongozi wa chama cha siasa unaopatikana kwa rushwa hauwezi kukemea rushwa wala matendo mabaya katika jamii", ameandika Lema.
Lema ametoa wito kwa wajumbe wa CHADEMA kuhakikisha kuwa uchaguzi wa uongozi unazingatia maadili na matendo mema. Amesisitiza kuwa, "Tukiuua maadili ya wanachama wetu, hatuwezi kuwa na ujasiri wa kudai haki."
Ameshauri wajumbe kumchagua Tundu Lissu kwa nafasi ya uenyekiti, akisisitiza kuwa ni muhimu kuchagua viongozi kwa misingi ya uadilifu badala ya kufuata rushwa au maslahi binafsi.