Lema: Unazuia impression ya wanachama wako kuja katika maeneo ya uchaguzi mkuu ndani ya chama? Hadi unaweka walinzi binafsi?

Lema: Unazuia impression ya wanachama wako kuja katika maeneo ya uchaguzi mkuu ndani ya chama? Hadi unaweka walinzi binafsi?

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter), Lema ameonesha kushangazwa na mwelekeo wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wake unaotarajiwa kufanyika kesho, Jumanne, Januari 21, 2025.

"Unazuia impression ya wanachama wako kuja katika maeneo ya uchaguzi mkuu ndani ya chama? Hadi unaweka walinzi binafsi? Tumeanza lini hii tabia ya kukataa wanachama wetu kwenye mazingira ya vikao vyetu?" aliandika Lema kwa mshangao.

Aidha, Lema amewataka wajumbe wa chama hicho kutafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi, akisisitiza kuwa viongozi ni Tundu na John Heche ndio watu sahihi wa kukivusha chama kutoka katika changamoto zilizopo.
 
Jamaa kashadata.....na kesho asije akavaa boxer kichwani akafikiri ni kofia.

Na hii ni baada ya Balaza kuu leo kubariki majina ya wale wahuni yasirudi nikajua hili ni PIGO KUU kambi ya Lissu.

Uchaguzi ushaisha huo.. mchwa kashakula kamba.....
 
Yeye Lema afanye kampeni watu wake wachaguliwe, ila sio kubagaza wengine
 
Hela ya kuleta Walinzi binafsi ipo kwenye shughuli nyingine za chama fedha hakuna.
 
Back
Top Bottom