johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Injinia Kagoshaki kutoka Japan ameshangaa inakuwaje mtu anayegombea uongozi wa serikali anajaza fomu kwa mkono!
Kagoshaki anasema Japan unapojaza fomu yoyote hata ya kuomba chumba cha kulala Hotelini utatumia kompyuta ambayo itakuwa inakupa mwongozo ili usikosee. Lengo la kujaza fomu ni kupata taarifa tarajiwa siyo " kumtega" mjazaji ili umuhukumu, amenielimisha mjapani.
Kule Japan mtu hawezi kukosea kujaza fomu hata kama amelewa kwa sababu fomu haikosewi.
Nawatakia mchana mwema!
Maendeleo hayana vyama!
Namwambia Daudi MchambuziMwambie Jafo sio sisi JF
Kweli wewe Kasuku,ulivyokaririshwa unavitema hivyo hivyo hata bila kuelewa mada husikaWafundishe hao CHADEMA
Nenda PM yakeNamwambia Daudi Mchambuzi
Kumbe akikuambia mjapani somo linatengamaa, lakini akisema Masiya hauelewi. Ndio maana nilisema wastarabu kwenye mambo ya msingi ya kitaifa hawategani.Lengo la kujaza fomu ni kupata taarifa tarajiwa siyo " kumtega" mjazaji ili umuhukumu, amenielimisha mjapani.
Hata mimi nakubaliana na wewe. Lengo la kujaza fomu ni kupata taarifa unayoitaka kutoka kwa mhusika. Fomu inatakiwa ieleweke kwa urahisi na mjazaji. Ukiona wajazaji wengi wanafanya makosa basi ujuwe wewe uliyeitoa fomu ndiyo mwenye kasoro. Na hata akama imekosewa lazima mtoa fomu atoe muda wa kufanya marekebisho. Baadhi ya makosa ambayo yanaweza kufanya fomu iwe batili ni fomu iliyokosewa/kujazwa taarifa za uongo au ilicholeweshwa kurudishwa baada ya muda uliowekwa kufika.I tend to agree. Huku africa kujaza fomu ni kama unafanya mtihani, mitego miingi.
Aiseeeee. Vichaaa wamejaa kila konaWafundishe hao CHADEMA