mwananthropolojia
JF-Expert Member
- Oct 6, 2012
- 956
- 657
Bunge saizi linaboa,ni la upande mmoja baada ya wenzao wa serikali 3 kutoka,ila naona wale wa serikali 2 wameachiwa nafasi na bado wanashindwa kujenga hoja ya namna kuitoa Tanzania kwenye umasikini wa miaka 50,wamebaki kung'ang'ania kero zinarekebishika ndani ya2.
Ajabu kwa miaka50 ndani ya serikali2 wamejaribu kutatua bila mafanikio. Serikali3 ilikua imejaa maono/vision kuliko muundo wa serikali2.
Huu muundo wa serikali2 hauna mvuto wa kuvutia hata nchi nyingine kujiunga.Mimi nilidhani muungano wetu na Zanzibar lengo lilikua wenzetu wa mataifa mengine ya kiafrika wavutiwe na muungano wetu ili nao wajiunge kidogodogo, mwisho afrika nzima iwe moja.
Hilo ndilo lilikuwa lengo la waasisi wetu kuungana,na ndio ubishani mkubwa uliokuepo kati ya Nyerere na Nkrumah.
Nyerere alitaka tuungane kidogodogo wakati Nkrumah alitaka umoja wa haraka wa Afrika.Huu muundo wa serikali 3 unaruhusu na unavutia nchi zingine zijiunge,kwa maana nyingine ni muundo endelevu,umekaa kiexpansionist.
Wengi tumesahau lengo la kuungana hasa ilikua nini . Mwanzo mipango ilikuwa kuiunga East africa ndio iwe mfano kwa Afrika nzima kujiunga kua pamoja,wakenya na waganda wakalikataa kwa kipindi kile.
Nyerere alipoona imeshindikana akawageukia wazanzibar ili uwe muungano wa mfano.Sasa ni miaka50 imepita ndio tumeungana,je tumefanikiwa kuwashawishi wenzetu wajiunge nasi kwenye huu muungano?jibu ni hapana,kwa miaka50 tumeshindwa kuwashawishi.
Tujiangalie sasa tunaungana kwajili gani?.Kama ni kwajili ya ulinzi na undugu tujue, maana kama ni suala la kiuchumi basi hamna faida, muungano umekua ukiongeza gharama tu kwani ni sisi wananchi wa Tanganyika ndio tunaingia gharama na sio wenzetu wazanzibar.
Mapato tunayopata kutokana na muungano ni madogo kuliko matumizi. Tukiangalia hii miundo, Serikali3 imekaa kiuwazi na kiuwajibikaji wa matumizi ya rasilimali na uongozi,kwa maana nyingine una faida kiuchumi,kwani uchumi ni matumizi mazuri ya rasilimali ulizonazo kwa mpangilio mzuri.
Wakati serikali2 imekaa kisiasa zaidi na hautaki mabadiliko kwa mana nyingine aliye masikin ataendelea kua masikin na aliye juu atazidi kua juu.
Serikali1 imekaa kiulinzi na kindugu zaidi,ila tatizo wazenj washasema sisi ni watu tofauti,kwaio serikali moja itazid kuleta mgogoro.
Turudi kwenye lengo halisi.