Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Hakuna nchi hata moja inayopenda kuwa masikini duniani, lakini tatizo kubwa linakuja kwenye kujua mbinu gani zitumike ili kuhakikisha umasikini huu unatokomezwa kabisa. China ilikuwa na ndoto ya kutokomeza umasikini tangu kilipoasisiwa chama cha Kikomunisti cha China mwaka 1949. Ingawaje kasi ya awali ya kuondoa umasikini inatofautiana na hii ya sasa, lakini ndoto hii imeshuhudiwa ikiendelezwa na viongozi wa awamu zote hadi kufikia sasa.
Tarehe 29 Novemba, mwaka 2015, chini ya uongozi wa rais Xi Jinping wa China, kampeni ya kutokomeza kabisa umaskini ikaanza nchini China. Na toka hapo juhudi hizi zimeleta maajabu makubwa. Mwaka 1990, kulikuwa na watu zaidi ya milioni 750 wanaoishi na umasikini katika nchi nzima ambao ni zaidi ya 60% ya watu wote wa China. Na karibu miaka 30 baadaye yaani mwaka 2019, idadi hiyo imepungua hadi milioni 16.6 kwa hiyo tunaweza kusema kuwa China imeingia kwenye enzi mpya ya kupunguza umaskini.
Katika kipindi cha miaka sita iliyopita, idadi ya watu wanaoishi na umasikini imepungua kutoka milioni 98.99 mwishoni mwa 2012 hadi milioni 5.51 mwishoni mwa mwaka 2019. Kiwango cha umaskini kimepungua kutoka asilimia 10.2 hadi asilimia 0.6, na idadi ya watu maskini imepungua kwa zaidi ya milioni 10 kila mwaka kwa miaka minane mfululizo.
China imepanga kukamilisha kazi ya kuondokana na umasikini katika maeneo ya vijijini mwaka huu wa 2020, na hiyo ni ahadi iliyotolewa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambayo ni lazima itimizwe kwa wakati uliopangwa. Hivyo China itajenga jamii yenye maisha bora katika pande zote, na kutambua ndoto na matarajio ambayo taifa la China limekuwa likifuatilia kwa maelfu ya miaka. Hata Benki Kuu ya Dunia imesema hili ni moja ya tukio kubwa katika historia ya binadamu.
Mpango wa serikali ya China wa kuondoa umasikini umegawanyika katika mikakati miwili yaani sera kubwa za taifa na hatua za kuchukuliwa na serikali za miji.
Katika ngazi ya taifa sera hizo zinahusu matumizi kwenye miundo mbinu. Uongozi wa rais Xi umetoa mabilioni ya yuan kuondoa tatizo hilo. Na sasa zimeshuhudiwa barabara zenye zaidi ya kilomita 200,000 zikijengwa au kukarabatiwa katika mwaka 2018 na 94% ya vijiji masikini vikiunganishwa na mtandao wa internet.
Mbali na hapo makampuni kadhaa ya serikali yamejiunga kwenye kampeni na kutoa yuan bilioni 30 kwenye mipango ya kuondoa umasikini mapema mwaka 2019.
Lakini kwa kiasi fulani, kampeni ya kupambana na umasikini imeachwa mikononi mwa maafisa wa ngazi za chini pia. Kila afisa wa ngazi ya mji anakwenda kwenye kaya na kujaribu kujua kinachoendelea na kwanini watu ni masikini, na hatimaye jinsi gani ya kutumia rasilimali kuondoa hali hiyo.
Ufumbuzi unaopendekezwa unatofautiana lakini mara nyingi wanazingatia kuwahamasisha wanakijiji kujiondoa kwenye umasikini kwa kuanzisha viwanda, kushiriki kwenye biashara ya kwenye mtandao na kuongeza utalii wa maeneo ya vijijini.
Katika kijiji cha kabila la Washe, ili kuongeza mapato ya wanakijiji, kamati ya kijiji imejiandikisha, kukarabati, na kukodisha nyumba za zamani za wanakijiji, na kuanzisha hoteli kwenye nyumba hizi. Baada ya maendeleo ya miaka kadhaa, kijiji hicho kimekuwa na sura mpya, na maisha ya watu yameboreka zaidi.
Licha ya hayo, kijiji cha Zhongcun, mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China kimepata njia mpya ya kuondokana na umasikini, ambayo ni kilimo cha dawa za jadi za China zenye soko kubwa. Na kila mwanakijiji anayelima dawa hizo, anaweza kupata dola za Kimarekani 15 kwa siku.
Ingawa nchi nyingi za Afrika zinajitahidi kupambana na umasikini lakini kasi yake inaonekana bado ni ndogo. Baadhi ya nchi kama Tanzania sasa zimeweza kuinua hata kiwango chake cha uchumi na kuondokana na umasikini uliokithiri kwa kuanzisha mifumo wezeshi inayowafanya wananchi kuacha kubweteka na badala yake kufanya shughuli za kuwaongezea kipato.
Mfano mzuri ni wilaya ya Makete ambayo ni miongoni mwa halmashauri zinazotekeleza mpango wa kunusuru kaya maskini kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). Mpango huo umesaidia kuzinusuru kaya maskini ambapo wengi wao walikosa uhakika wa chakula, malazi na hata elimu hali iliyosababisha uchumi wa familia nyingi kudidimia. Mbali na hapo serikali ya Tanzania imeanzisha miradi mingine mingi ya kuwainua wananchi pamoja na nchi kwa ujumla ikiwemo ya barabara, reli, mashule, mahospitali, kilimo, utalii, kutoa nafasi nyingi za ajira n.k.
Hivyo kama nilivyosema awali kwamba kila nchi inajitahidi kupambana na kutokomeza umasikini ingawa ni kwa kutumia njia na mbinu tofauti lakini zote zina lengo moja.