Mimi naanza na mkasa wa Zitto Kabwe! Alikuwa machachari miaka ile akiwa Chadema. Akatuhumiwa kuongea uongo bungeni. Basi aliyepata kuwa Mbunge wa Mchinga, Mudhihir M. Mudhihir akatoa muongozo wa namna Zitto anavyopaswa kushughulikiwa huku akimnyooshea mkono.
Zitto akala ban bungeni, siku chache baadae Mudhihir akapata ajali na kukatika ule mkono aliotumia kumnyooshea Zitto.